JAMAA ABAMBWA AKIWA NA MITAMBO YA KUWAIBIA AZAM NA ZUKU.

 
Stori: Chande  Abdallah na Deogratius mongela
Katika hali ya kushangaza, mtu mmoja anayefahamika kwa jina la Ali, mkazi wa Mwananyamala jijini Dar, amekamatwa na polisi baada ya kudaiwa kuunganisha visivyo halali, mitambo ambayo iliwawezesha watu kuangalia matangazo ya televisheni ya vituo mbalimbali kwa malipo rahisi.
Bw. Ali anayedaiwa kuunganisha visivyo halali, mitambo ya kurusha matangazo ya televisheni ya vituo mbalimbali kwa malipo rahisi.
Awali, msamaria mwema mmoja alipiga simu kwa kikosi kazi cha Operesheni Fichua Maovu (OFM) cha Global Publishers na kukitonya juu ya uwezo wa mtu huyo anayewashangaza kwa utaalamu wake wa kuunganisha mitambo hiyo bila kugundulika.
Baadhi ya ving'amuzi vilivyokuwa vikitumiwa na mtuhumiwa kuunda mtambo wa mawasiliano.
“Hapa kuna watu kama 80 hivi wameunganishwa, wanaangalia televisheni za Azam, Zuku na nyingine kwa bei chee, lakini wanaangalia mipira, filamu na kila kitu, yaani huwezi kuamini kaka,” chanzo hicho kilinyetisha kwa OFM.
Bw. Ali (kushoto) akibanwa kwa maswali juu ya biashara haramu anayofanya.
Katika kujiridhisha, kikosi kazi chini ya kamanda mkuu, kilitembelea eneo la tukio na kufanya ukaguzi wa siri, uliothibitisha kuwepo kwa huduma hiyo, lakini bila ya kuwepo kwa dekoda za vituo hivyo vya televisheni vinavyotolewa kwa malipo.
Ulinzi mkali ukiimarishwa nje ya nyumba ya Bw. Ali.
Baada ya kujiridhisha huko, OFM ilifanya mawasiliano na wahusika wa vituo hivyo, ambao nao walitembelea eneo hilo la tukio na kujionea wenyewe. Wahusika hao walikuwa ni Afisa Leseni wa DSTV na Afisa Mauzo wa Azam Tv pamoja na mtu mmoja kutoka chama cha hakimiliki cha COSOTA.
Afisa Leseni kutoka chama cha hakimiliki COSOTA, Zephania Lyamuya (kulia) akisimamia zoezi.
OFM iliwashauri maofisa hao kuripoti jambo hilo kituo cha polisi, ushauri ambao waliukubali na kwenda kutoa taarifa Kituo cha Polisi Oystebay ambao waliongozana na watu hao hadi Mwananyamala.
Madishi ya Satelaiti yanayotumiwa na Bw. Ali kurushia matangazo ya televishen yakiwa juu ya nyumba yake.
Kufika nyumbani kwa mtuhumiwa huyo ambaye pia ni maarufu kwa jina la utani kama Masetelaiti, Polisi walifanikiwa kumkamata na baada ya upekuzi, waligundua kuwepo kwa mitambo ya aina mbalimbali, vikiwemo ving’amuzi vya aina mbalimbali, modulators, Receivers na vifaa vingine vikionekana vikiwa vimeunganishwa kwa utaalamu wa hali ya juu katika ukuta wa sebule yake.
Afisa Mkuu wa Mauzo kutoka kampuni ya Azam, Shah Seffu akiwa nje ya ofisi ya Bw. Ali.
Masetelaiti alikiri kuendesha maisha kwa staili hiyo na kudai kuwa utaalamu wa kuunganisha ving’amuzi hivyo ni wake mwenyewe na amekuwa akifanya hivyo kwa muda mrefu.
Afisa Leseni kutoka Cosota, Zephania Lyamuya alisema jamaa huyo anastahili kupelekwa Polisi kutoa maelezo kwani licha ya kutokuwa na leseni ya kufanya biashara hiyo, pia amekuwa akiwanyonya waigizaji wanaostahili kulipwa kila filamu zao zinaporushwa katika televisheni za nje.
Kikosi kazi kikifungua mitambo na kuharibu kazi haramu ya Bw. Ali.
Naye Afisa Mkuu wa Mauzo kutoka kampuni ya Azam aliyejitambulisha kwa jina la Shah Seffu (pichani kulia), alisema kuwa operesheni hiyo ni moja kati ya hatua walizozipanga kumaliza tatizo la kuingilia mawasiliano ya televisheni jambo ambalo limeonekana kukua kwa kasi nchini.
Baadhi ya Ving'amuzi vilivyokusanywa kutoka katika mtambo uliosukwa na Masatelaiti.
Baada ya kuvikusanya vifaa hivyo vilipelekwa katika Kituo cha Polisi cha Oysterbay sambamba na mtuhumiwa kutoa maelezo ambapo jalada lilifunguliwa OB/RB/16106/2014, KUINGILIA MAWASILIANO YA TELEVISHENI

chanzo:globalpublishers

Comments

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA