WANACHUO 58 WAPOTEA MEXICO

Mama wa mmoja wa wanachuo walotoweka
Polisi wa kusini mwa Mexico katika mji wa Guerrero wanawasaka wanachuo 58 wa chuo cha ualimu ambao hawajulikani waliko tangu yalipotokea mapigano baina ya polisi na wanachuo hao mwishoni mwa wiki .

Wanafunzi hao ni kutoka katika chuo cha ualimu inasemekana walitoweka baada ya kukabiliana na polisi wakati wa maandamano.

Katika makabiliano hayo na askari watu sita walipoteza maisha na wengine kumi na saba walijeruhiwa wakati mtu mwenye silaha alipowashambulia waandamanaji hao na abiria waliokuwa kwenye basi katika kijiji cha Iguala.

Wanachuo hao wa chuo cha ualimu waliinggia kwenye maandamano kupinga upendeleo wa wanachuo wenzao wa mjini kupendelewa zaidi katika nafasi za mafunzo kazini kuliko wa kutoka vijijini.

chanzo:BBC

Comments

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA