SERIKALI ITAHAKIKISHA VIFAA VINAPATIKANA
Mahmoud Ahmad Arusha
Serekali
imesema kuwa itaendelea kuhakikisha vifaa vya mamlaka ya hali ya hewa
vinakuwa vya kisasa zaidi huku ikiwataka watanzania kufuata utabiri wa
hali ya hewa kwani inawasaidia kujua hali ya hewa kwa faida yao ya
kiamaendeleo.
Kauli
hiyo imetolewa na naibu waziri wa uchukuzi dkt Chalres Tibeza wakati
akifungua mkutano wa wakuu wa mashirika ya hali ya hewa wa nchi
wanachama wa SADC unaofanyika jijini hapa huku akiwataka kuhakikisha
viwango vya utabiri kwa nchi hizo vinakuwa ilikuendana na changamoto
zilizopo.(Martha Magessa)
Tibeza
alisema kuwa Taarifa za hali ya hewa ni muhimu kwa maendeleo ya kiuchumi
kwani zinasaidia kujua kesho itakuwa na hali gani ya hewa vile vile
inamsaidia hata mkulima,mvuvi na wote kwani inasaidia kwenye maeneo
mengi hata wasafiri wanaoenda kwenye biashara zao wakisafiri kwa kutumia
ndege pia zinawasaidia hivyo ni wajibu kwa kila mwananchi kuzifuatilia
na si kuzibeza.
Alisema
kuwa kwa sasa utabiri wa hali ya hewa hapa nchini umefikia kiwango cha
Asilimia 85% na wakahakikisha kuwa maeneo mengi yanakuwa na vifaa vya
kuwawezesha kutoa utabiri kwa asilimia mia utakaosaidia kukua kwa sekta
hiyo muhimu kwa maendeleo ya taifa.
Nae
Mkurugenzi wa miundombinu na huduma wa jumuiya hiyo(SADC) Remmy Makumbe
alisema kuwa nchi hizo zinachangamoto kubwa ya kukabiliana nao ikiwemo
uhaba wa vifaa utakaosaidia kukuwa kwa viwango vya kimataifa ya utabiri
wa hali ya hewa,na kubadilishana uzoefo ikiwemo mbinu mpya za
kukabiliana na chngamoto zinazozikabili nchi wananchama.
Alisema
kuwa pamoja na changamoto mbali mbali zinazoikabili jumuiya hiyo ikiwemo
michongo kutotolewa kwa wakati nan chi wanachama pia mkutano huo
unajadili mapendekezo yatakao pelekwa kwa mawaziri wan chi hizo kupitia
mapendekezo hayo.
Aidha kwa
upande wake Mkurugenzi mkuu wa mamlaka ya hali ya hewa TMA hapa nchi
Dkt.Agnes kijazi alisema kuwa kukuwa kwa setka hiyo ya utabiri wa hali
ya hewa hapa nchini kunatokana na kuwa na vifaa vya kisasa vinavyosaidia
utoaji wa utabiri wenye viwango na kuishauri serekali kusaidia
upatikana wa vifaa zaidi kwenye sekta hiyo.
Dkt
Kijazi alisema kuwa mkutano huo mkuu wan chi wanachama wa sekta ya hali
ya hewa wa jumuiya ya maendeleo ya nchi za kusini SADC ni mkutano wa
kuratibu mapendekezo yatakayo wasilishwa kwa mawaziri na baadae kwa
wakuu wan chi wanachama.
Alisema
kuwa Idara hiyo inasaidia sana kisayansi kujua hali ya hewa ikiwemo
utunzaji wa mazigira ambayo yanasaidia kutobadilika kwa hali ya hewa ya
eneo Fulani la nchi hivyo kuweza kuyaboresha mzingira yetu huku
akiwataka wananchi kutunza mazingira kwa faida ya kutobadilika kwa hali
ya hewa kwenye maeneo yao.
Comments
Post a Comment