MALISA GODLISTEN: KULIKONI UWEPO WA MAKAMU WA RAIS WATATU KATIKA NCHI MBILI?

Kutoka katika account ya facebook ya ndugu Malisa  Godlisten nimekutana na maswali yenye mantiki na hoja za msingi ambazo msomaji na mfatiliaji wa blog hii unapaswa nawe kujiuliza.
Endelea kufatilia alichokiandika kuanzia aya inayoanza;
 
"Pamoja na marekebisho mengi yaliyofanywa kwenye Rasimu, kwa kuondoa vipengele vya msingi na kuweka vya hovyo, leo ninahoji vipengele viwili tu na kesho nitaendelea.

Mosi,Kama walisema hatuwezi kuwa na Marais watatu ktk nchi mbili, wamewezaje kuweka Makamu wa Rais watatu katika nchi mbili?? Mbona kama ni contradiction?

Pili, ni kuhusu wabunge. Kwanini Rasimu ya Sitta imekataa wabunge wasiwajibishwe pale wanaposhindwa kuperform? Ina maana mbunge akiwa mzigo wananchi hawana cha kufanya hadi miaka mitano ipite?? This is typical unfair.

Na pia kwanini ukomo wa wabunge umeondolewa? Wananchi walisema vipindi vitatu tosha, ili watu wengine nao wapate fursa ya kuonesha talent zao za uongozi. Lakini Sitta kasema Ubunge hauna kikomo. Kikomo chake ni kifo. 

Ukiwa mbunge ukiwa na miaka 25 unaruhusiwa kuendelea kuwa mbunge hata ukifikisha miaka 100, ili mradi tu ugombee na ushinde. This is also unfair kwa wananchi. Hivi vijana wenye charisma ya uongozi watapata lini fursa ya kutumikia taifa kama vikongwe wataendelea kuongoza hadi watakapoondolewa na mauti"
‪#‎Nawaza_tu_kwa_sauti‬.

Comments

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA