PICHA: KANYE WEST AFUNDISHA CHUO KAMA SEHEMU YA KUTUMIKIA KIFUNGO CHA NJE

Kanye West1 
Rapper Kanye West anatumikia kifungo cha nje baada ya kumpiga paparazi mwaka 2013, hukumu ilipotolewa alipewa kifungo cha nje kama adhabu kwa kosa alilotenda, adhabu hiyo inaenda sambamba na kuitumikia jamii kwa muda wa masaa 250. Kanye anatumia masaa hayo kufundisha na kuongea na wanafunzi wa chuo cha L.A. Trade Technical College kama sehemu yake ya hukumu.
 
Kanye West amekuwa akitumia masaa hayo katika kuongea na wanafunzi wa chuo hicho kwa kuwaeleza uzoefu wake katika tasnia ya fasheni za nguo pamoja na muziki.
picha zikimuonyesha Kanye akiwa darasani akifundisha.




 

Comments

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA