NAFASI ZA KAZI KOPLO NA KONSTEBO WA UHAMIAJI ZIMETANGAZWA TENA, SOMA HAPA

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi anatangaza nafasi za kazi
zifuatazo katika Idara ya Uhamiaji kwa Raia wote wa Tanzania wenye sifa.

1. KOPLO WA UHAMIAJI Nafasi 114 - (Nafasi 100 kwa ajili ya Tanzania
Bara na Zanzibar na nafasi 14 maalum kwa ajili ya Zanzibar tu)

A.  SIFA ZA MWOMBAJI:
(i) Awe Raia wa Tanzania mwenye umri kuanzia miaka 25 hadi 30.
(ii) Awe  amehitimu  kidato  cha  sita  na  kufaulu  masomo  ya  Kiingereza,
Kiswahili,  Historia,  Jiografia,  Kifaransa,  Hisabati  ambapo  masomo
mawili kati ya hayo yawe katika kiwango cha “Principal”.
(iii) Awe pia na mojawapo ya sifa zifuatazo:
 Cheti cha Sheria;
 Cheti cha Kompyuta;
 Cheti cha Ufundi (FTC) kwenye fani ya umeme na mitambo
(iv) Waombaji  wenye  ujuzi  wa  mojawapo  ya  lugha  zifuatazo  (Kifaransa,
Kichina, Kijerumani, Kiarabu au Kihispania) watafikiriwa kwanza.
(v) Aidha, Mwombaji aliyepitia mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa atapewa
kipaumbele.

B. MAJUKUMU NA KAZI ZA KUFANYA

(i) Kusimamia upangaji wa majalada ya watumiaji wa huduma za uhamiaji;
(ii) Kusimamia ufunguaji wa majalada ya watumiaji wa huduma za uhamiaji
pamoja na majalada binafsi ya watumishi wa uhamiaji;
(iii) Kuandika hati mbalimbali za uhamiaji;
(iv) Kuwa viongozi wasaidizi wa makundi ya doria na ukaguzi;
(v) Kusindikiza watuhumiwa wa kesi za uhamiaji mahakamani pamoja na
wageni wanaofukuzwa nchini (Deportees)

2. KONSTEBO  WA  UHAMIAJI  Nafasi  114 
-  (Nafasi  100  kwa  ajili  ya
Tanzania Bara na Zanzibar na nafasi 14 maalum kwa ajili ya Zanzibar tu)

A. SIFA ZA MWOMBAJI:
(i) Awe Raia wa Tanzania mwenye umri kuanzia miaka 20 hadi 25.
(ii) Awe  amehitimu  kidato  cha  nne  na  kufaulu  masomo  ya  Kiingereza,
Kiswahili,  Historia,  Jiografia,  Kifaransa,  Hisabati  ambapo  masomo
matatu kati ya hayo yawe katika kiwango cha “Credit”.
(iii) Awe pia na mojawapo ya sifa zifuatazo:
 Cheti cha Sheria;
 Cheti cha Utunzaji Kumbukumbu;
 Cheti cha Kompyuta;
 Cheti cha Ufundi (FTC);
 Cheti  cha  Mafunzo  ya  Ufundi  Stadi  kwenye  fani  ya  (umeme,
mitambo, bomba);
(iv) Waombaji  wenye  ujuzi  wa  mojawapo  ya  lugha  zifuatazo  (Kifaransa,
Kichina, Kijerumani, Kiarabu au Kihispania) watafikiriwa kwanza.
(v) Aidha, Mwombaji aliyepitia mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa atapewa
kipaumbele.

B. MAJUKUMU NA KAZI ZA KUFANYA
(i) Kupanga majalada ya watumiaji wa huduma za uhamiaji;
(ii) Kufungua na kutunza majalada yenye orodha ya majina ya watumiaji wa
huduma za uhamiaji;
(iii) Kufanya doria sehemu za mipakani, bandarini, vituo vya mabasi, treni na
sehemu zenye vipenyo vya kuingia na kutoka nchini;
(iv) Kukamata  watuhumiwa  wa  makosa  mbalimbali  ya  uhamiaji  na
kuwafikisha kwenye mamlaka husika;
(v) Kufanya ukaguzi kwenye hoteli, nyumba za kulala wageni na sehemu za
biashara;
(vi) Kusindikiza watuhumiwa wa kesi za uhamiaji mahakamani pamoja na
wageni wanaofukuzwa nchini (Deportees)
(vii) Kufanya  matengenezo/ukarabati  wa  mitambo  na  vitendea  kazi  vya
uhamiaji;
(viii) Kuandaa hati mbalimbali za uhamiaji.
2
3. UWASILISHAJI WA MAOMBI
Barua za maombi zinapaswa kuandikwa kwa mkono na kuwasilishwa kwa njia
ya posta zikiwa zimeambatishwa na:-(i) Nakala ya cheti cha kuzaliwa;
(ii) Nakala ya cheti cha kuhitimu masomo ya sekondari pamoja na vyeti kwa
mujibu wa sifa nyingine zilizoainishwa kwenye kipengele A(iii). (result
slipshazitakubalika)
(iii) Nakala ya vyeti vya kumaliza shule ya msingi na sekondari  (Leaving
Certificates);
(iv) Picha mbili (Passport Size);
(v) Barua  ya  Utambulisho  kutoka  kwa  Mwenyekiti  wa  Serikali  za
Mitaa/Shehia/ Vijiji;
(vi) Nakala  za  vyeti  vyote  vitakavyowasilishwa  viwe  vimethibitishwa  na
Wakili/ Kamishna wa Viapo.

4. ANUANI YA KUWASILISHA MAOMBI
Barua za maombi ya kazi ziwasilishwe kwa njia ya posta  ndani ya kipindi cha
siku 14 kuanzia tarehe ya tangazo hili kwa anuani zifuatazo:- Waombaji wa nafasi 200 (100 Koplo na 100 Konstebo) ambazo ni
kwa ajili ya Tanzania Bara na Zanzibar wawasilishe maombi yao
kwa anuani ifuatayo:

Katibu Mkuu,
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,
S.L.P 9223,
DAR ES SALAAM.

 Waombaji wa nafasi   28 (14 Koplo na 14 Konstebo) ambazo ni
maalum  kwa  Zanzibar  wawasilishe   maombi  yao  kwa  anuani
ifuatayo:
Katibu Mkuu,Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,
C/O Kamishna wa Uhamiaji Zanzibar,
S.L.P 1354,
ZANZIBAR.

Maombi  ambayo  hayatazingatia  maelekezo  tajwa  hapo  juu
hayatashughulikiwa.
3
FUNGUA TANGAZO

Comments

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA