JARIDA LA FORBES LAMTAJA DR. DRE KUWA MSANII WA HIP HOP MWENYE MKWANJA MREFU WA $ 620 MILLION;DRAKE & MACKLEMORE WAINGIA TOP 5




Jarida la Forbes limetoa orodha mpya ya mwaka mzima ilianziwa kufanyiwa kazi kuanzia June 2013- June 2014 ili kuweza kupata wasanii wa hip hop ambao wanapesa nyingi kulingana na shughuli wanazozifanya za kimuziki ikiwemo mikataba minono waliosaini na makampuni mengine, uuzaji wa album, tours, pamoja na mali wanazo miliki.

Kwa mara ya kwanza Dr. Dre amewapiku Jay Z na Diddy ambao wamekuwa vinara wa muda mrefu katika nafasi hiyo ya kwanza, Dr. Dre anashikilia nafasi hii kwa mara ya kwanza mara baada ya kupata deal kubwa ya kuuza kampuni ya Beats electronics kwenda kwa Apple ambaye yeye ni mmoja wapo wa waanzilishi wa kampuni hiyo, ambapo iliuzwa kwa dola za kimarekani Billion 3 na kuweza kumpa nguvu Dr. Dre kuwaburuza wasanii wenzake kwa kuwa na mkwanja mrefu.sana wa dola 620 millioni huku anayemfata akiwa na dola 60 million.

Orodha kamili ya wasanii wengine hii hapa.
1. Dr. Dre – $620 million
2. Jay Z – $60 million
2. Diddy – $60 million
4. Drake – $33 million
5. Macklemore & Ryan Lewis – $32 million
6. Kanye West – $30 million
7. Birdman – $24 million
8. Lil Wayne – $23 million
9. Pharrell Williams – $22 million
10. Eminem – $18 million
11. Nicki Minaj – $14 million
12. Wiz Khalifa – $13 million
13. Pitbull – $12 million
14. Snoop Dogg – $10 million
15. Kendrick Lamar – $9 million
16. Ludacris – $8 million
16. Tech N9ne – $8 million
16. Swizz Beatz – $8 million
16. 50 Cent – $8 million
20. Rick Ross – $7 million
20. J. Cole – $7 million
20. DJ Khaled – $7 million
20. Lil Jon – $7 million
20. Mac Miller – $7 million

chanzo:allhiphop.com


Comments

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA