WACHUNGAJI MBARONI KWA KULAWITI WATOTO

Stori: Joseph Ngilisho, Arusha
WATOTO sita, wakiwemo wawili wa kiume wenye umri wa miaka 8 hadi 14 wameharibiwa vibaya sehemu zao za siri baada ya kubakwa kanisani na watu wanaodaiwa ni wachungaji.
Watoto sita waliobakwa kanisani na watu wanaodaiwa ni wachungaji.
Wakiwa katika Hospitali ya Mkoa wa Arusha, Mount Meru walikopelekwa kwa matibabu na kuangaliwa maambukizi ya magonjwa ya zinaa, watoto hao walidai kufanyiwa mchezo huo kwa nyakati tofauti  na wachungaji watatu wa kanisa hilo lililopo eneo la  Feed Force, Kwamorombo jijini Arusha.

Mmoja wa watoto hao anayesoma darasa la 4 katika shule ya msingi alieleza kuwa yeye na wenzake wamekuwa wakifanyiwa mchezo mchafu katika kanisa hilo baada ya wachungaji hao kuwapatia shilingi 2,000 za kufungia mdomo.

“Siku moja nilipofika shuleni wenzangu wakaniambia niende pale kanisani tukapewe hela, nilipofika niliwaona wenzangu wengine wakifanyiwa mchezo mchafu na mimi mchungaji aliniambia niiname akanifanyia kitendo kibaya na kunipa shilingi 2,000, niliumia sana,’’ alisema mwanafunzi mmoja.

Mwanafunzi mwingine alisema amekuwa akitoroka shuleni na wenzake na kwenda kwa watumishi hao ambapo huwaingiza katika kanisa hilo na kujifanya wanawaombea baadaye huwafanyia mchezo mbaya.

Chanzo:global publishers

Comments

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA