PICHA: HONG KONG BADO HALI TETE

Raia wa Hong Kong wakivurumushiwa moshi
Makumi kwa mamia ya waandamanaji wa Hong Kong wanaendelea na maandamano yao kwa siku nyingine tena baada ya kudhoofisha maeneo muhimu ya jiji hilo wakati wa mchana. Waandamanaji hao sasa wanamtaka Mkuu wa utawala wa Hong Kong Leung Chun-Ying ajiuzulu..

Wakati huo huo Marekani imesema inafuatilia kwa karibu kinachoendelea Hong Kong na imeutaka utawala kuchukua hatua. Katika mkutano wa wanahabari msemaji wa Ikulu ya Marekani Josh Earnest amesema Marekani inaunga mkono matakwa ya watu wa Hong Kong.

"Duniani kote, na hii ni kweli katika Hong Kong na maeneo mengine, Marekani inaunga mkono kimataifa, uhuru, kama vile uhuru wa kukutana kwa amani na uhuru wa kujieleza. Marekani inautaka utawala wa Hong Kong kuchukua hatua, na kwa upande wa waandamanaji kutoa maoni yao kwa amani"

chanzo:bbc

Comments

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA