Ahuzunishwa picha zake za uchumba kuhusishwa na jambazi

22 Apr 2015

Hii ni moja ya picha inayomfananisha na Mwansheria

Mtumishi mmoja wa umma ambaye ni Mwanasheria wa Serikali amehuzunishwa na picha za tukio lake la kumvisha pete ya uchumba, mkewe mtarajiwa kusambazwa katika mitandao ya kijamii tokea jana zikidai ndiye mmoja wa majambazi yaliyokamatwa katika tukio la kupora mtalii hapo jana jijini Dar es Salaam.

Watu wamekuwa wakipotosha jamii kwa kuweka picha zisizo zake zikifananishwa naye. 

Katika kipindi cha "Leo Tena" cha Clouds FM, mwanasheria huyo amekanusha kuwa jambazi aliyekamatwa na kusisitiza kuwa yeye ni raia mwema na anaendelea kulitumikia taifa kama kawaida wakati majambazi hao wanashikiliwa na jeshi la polisi.


Aliyezungushiwa duara jeusi ni mtuhumiwa wa ujambazi aliyekamatwa jana
(huyu ndiye anayefananishwa na mwanasheria)


"Hapo jana mara baada ya tukio hilo kutokea la kuwakamata majambazi hao, nilipigiwa simu na watu mbalimbali wa karibu waliokuwa wakitaka kunieleza kusambaa kwa picha zangu katika mitandao mbalimbali ya kijamii nikifananishwa na jambazi na hivyo kutokana na mimi nilikuwa katikati ya kazi sikuweza kutambua mapema kitu kilichokuwa kikiendelea. Mara baada ya muda wa kazi kupita ndipo nilipoona picha zangu zinazofananishwa na huyo jambazi zikiwa zimesambaa kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii," alisema mwanasheria huyo. (via Pamoja Pure blog)
Picha ya anayefananishwa na jambazi

Moja ya ujumbe uliosambazwa kupitia WhatsApp ukisisitiza kuwa watu hao si wamoja, unasema:

mdogo wangu Usiisambaze hio picha tena uifute na uwataarifu na wa group hilo lingine .....huyo ni shemeji yangu last born wa mme wangu ni msaidizi mkuu wa jaji mkuu na bibi harusi anafanya kazi weight and measure ....na ndoa wame funga tarehe 12 / 04 /2015 manzese SDA church....taadhari jamani na sheria mpya iliopitishwa tunajiweka matatani wote.....waambieni na wengine sie mnaemfikiria kwamba ni jambazi

Picha za mtuhumiwa wa ujambazi akimvisha pete mchumba wake na picha za Mwanasheria katika vazi la arusi na mkewe ni matukio mawili tofauti.

Comments

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA