DIAMOND PLATINUMZ AMZUIA ZARI KUJIFUNGULIA A. KUSINI
Mama kijacho wake, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’.
Habari zilizonyakwa na Ijumaa Wikienda kutoka kwenye chanzo cha ndani ya familia ya Diamond zilieleza kwamba, tayari jamaa huyo amemuanzishia Zari kliniki Bongo.
Mkali wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ akiwa na mama kijacho wake, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’.
“Yaani Diamond hataki kabisa Zari kwenda kujifungulia South Africa (Sauzi). Anataka kila kitu kifanyike hapahapa Bongo. Tayari amemuanzishia kliniki kwenye Hospitali ya AMI (ipo Masaki, Dar),” kilitonya chanzo hicho.Mkali wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ akiwa na mama kijacho wake, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’.
Akizungumzia ishu hiyo, Diamond alisema kuwa anatamani kuwa karibu na mama kijacho wake huyo hivyo ni kweli anataka mwanadada huyo ajifungulie Bongo.
Diamond au Baba Kijacho alisema lengo la kufanya hivyo ni ili iwe shangwe kwa familia nzima tofauti na atakapojifungulia nje ambapo familia italazimika kusafiri kwenda kumuona Chibu Junior.
Kwa mujibu wa Diamond, Zari ambaye ni mama wa watoto watatu akifukuzia huyo wa nne
anatarajia kujifungua kati ya mwezi Julai au Agosti, mwaka huu.
chanzo:GPL
Comments
Post a Comment