KIMENUKA: MKE WA SHETTA ADAI TALAKA KISA ROSE NDAUKA

Staa wa Bongo Fleva anayesumbua na wimbo wa Shikorobo, Nurdin Bilal ‘Shetta’ akiwa na mkewe.
Alhamisi iliyopita, Shetta na Rose waliripotiwa na gazeti ‘dugu’ na hili la Amani kuwa walilala katika chumba kimoja katika Hoteli ya Kingway iliyopo mkoani Morogoro walipokuwa wamekwenda kwenye mazishi ya muasisi wa Kundi la Tip Top Connection, Abdul Bonge.
Kwa mujibu wa chanzo makini, mara baada ya gazeti hilo kusambaa mtaani na mke wa Shetta kufikishiwa nakala yake na wapenda ‘ubuyu’, kilinuka ile mbaya nyumbani kwa Mbongo Fleva huyo, Kijitonyama jijini Dar ambapo mwanamke aliamua kudai talaka yake.
Mke huyo wa Shetta ambaye wamebahatika kupata mtoto mmoja na msanii huyo (Kayla) alimjia juu mumewe na kutaka amwambie ukweli wa habari hiyo jambo lililoleta tafrani hadi kufikia hatua ya kutimka nyumbani hadi wazazi wa pande zote mbili wakalazimika kuweka vikao vya usuluhishi.
Licha ya jitihada hizo kutoka kwa wazazi, bado mama Kayla alikataa kusuluhishwa na kudai hasira zake zitashuka mara atakapokutana na Rose uso kwa uso.“Kilinuka kiasi cha mke wa Shetta kufungasha virago huku akisisitiza kwamba kabla ya kuondoka mazima atahakikisha anamfungia kazi Rose ili aweze kumweleza kinaga ubaga juu ya ilikuwaje akapindua na mumewe chumba kimoja,” kilisema chanzo.
Mwigizaji Rose Ndauka.
Wanahabari wetu walimtafuta Rose na kumuuliza kama amepata taarifa za kutafutwa na mke wa Shetta na kuhusu kuhusishwa na tukio hilo ambapo alijibu kuwa hajapata taarifa.“Mimi sijapata hizo taarifa, kama ananitafuta mimi nipo tu maana sijafanya kosa lolote. Kama nilivyosema awali, kweli nilisafiri na Shetta kwenda Morogoro na tulilala hoteli moja lakini vyumba tofauti, Shetta namheshimu siwezi kufanya naye jambo kama hilo,” alisema Rose.
Mapaparazi wetu baada ya kumalizana na Rose, walimvutia waya Shetta ili kujua ukweli wa tukio hilo ambapo alikiri kumtokea na kuwashushia lawama wambeya.“Ni kweli mke wangu amekerwa sana na habari zile, kuna wambeya ndiyo wamemjaza maneno kiasi cha kuleta tafrani hadi wazazi kuingilia kati ingawa mimi naamini haya ni mambo ya kifamilia tu ambayo mke wangu atayaelewa na yataisha tu.
“Mke wangu ni muelewa sana, nampenda na ananipenda, hii hali ni ya kawaida kwa wanandoa ila kwa kuwa mimi ni msanii mke wangu atajua tu kuwa watu wanaongea sana juu yetu,” alisema Shetta.

chanzo:GPL

Comments

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA