Mkutano wa kuimarisha biashara katika mpaka wa Mtukula

MTUKULA - MISSENYI 
 



Mkutano huu ambao unafanyika kwa siku mbili tarehe 16-17 April 2015, una lenga kusikiliza kero za wafanya biashara wanaotumia mpaka huu, kwani mpaka huu wa mtukula ni moja wapo ya mpaka ambao umekuwa gumzo kwa wafanya biashara kutoka Uganda kuja Tanzania au kutoka Tanzania kwenda nchini Uganda.

Moja wapo ya matatizo makubwa yaliyopo ni utitili wa vizuizi vya barabarani kwani kwa mfano halisi, kutoka mtukula hadi Bukoba vipo vizuizi vya barabarani maarufu kama BERIA 7 ambapo mtukula penyewe zipo beria 3 moja ikisimamiwa na TRA, ya pili ikisimamiwa na Halmashauri ya wilaya ya Missenyi na ya tatu ikisimamiwa na Jeshi la Polisi. Kyaka zipo beria 3.

Hata hivyo, mkoa wa Kagera unaongoza kwa kuwa na vizuizi vya barabarani (beria ) jambo ambao linatia hofu hata kisaikolojia kwanini uwepo wa vizuzi hivi. Waweza kufikiri kuwa ni kwa sababu ya kulinda usalama wa wananchi au wasafiri na mali zao, na pengine baadhu hufikiri kuwa na vizuzi vingi barabarani kunachochea ukuaji wa biashara!

Mkutano umehudhuria na wajumbe kutoka umoja wa Afrika Mashariki, wa Uganda na Tanzania. Baada ya mkutano huu wa Mtukula, mkutano mwingine utafanyika katika mpaka wa Sirari/ Isebania, katika mpaka wa Uganda na Kenya

Katika mkutano huo, Wafanyabiashara na wajasriamali wanaofanya shughuli za kibiashara katika mpaka wa Mtukula unaounganisha nchi ya Tanzania na Uganda wameomba mamlaka zinazohusika kuondoa urasimu na vikwazo visivyo vya kiforodha ili kuwaondolea usumbufu kwenye shughuli zao za kila siku.

Wito huo umetolewa na wafanyabiashara na wajasriamali hao katika semina iliyofanyika katika ukumbi wa jengo la Afrika Masharika liliopo Mtukula wamesema kuwa kuna vikwazo visivyokuwa vya kiforodha katika protoko ya soko la Afrika Mashariki vinasababisha kuwaingizia hasara wajasriamali kwani hata biadhaa zao hurabika na kupoteza thamani wakati wanatumia gharama kuzitafuta na kuzizalisha.

Mjasiriamali Kasongo Kitwana Mirambo kutoka mkoani Tabora amesema kuwa amelazimika kuishia mpakani na lengo lake lilikuwa auze karanga zake tani kumi nchini Uganda lakini ameshindwa baada ya kuwepo vikwazo ambavyo katika maelezo na protoko ya soko la Afrika Mashariki havijaainishwa kwenye sheria hivyo vimemsababishia hasara kubwa na kumwalibia malengo yake.

Pia amelalamikia ushuru unaotozwa kwenye bidhaa zinazosafirishwa akitolea mfano kuwa wakati anatokea mkoani Tabora alilipia ushuru wa mazao lakini alitozwa tena ushuru wa mazao alipofika Mtukula na kuongeza kuwa huko ni kumukandamiza mjasriamali na hawezi kupata faida na kufaidi uwepo wa soko la pamoja la jumuia ya Afrika Mashariki.

Ibrahimu Sekwaro ambaye ni mmiliki wa shule ya Lake View iliyopo Bukoba amesema kuwa kwa Tanzania kuna mlolongo mrefu unaoleta usumbufu kwa wataalamu kama walimu wanaotaka kuja nchini kufundisha kutoka nchi jirani ambazo ni mwanachama wa Jumuia mashariki wakati protoko ya soko la pamoja limeelekeza watu wenye ujuzi na kazi ataweza kuajiriwa bila vikwazo.

Amesema wakati nchi nyingine mwanachama wakitoa fursa hiyo kwa unafuu hali ni tofauti Tanzania ambapo mtu anayetaka ajira hiyo hulazimika kutafuta kibali cha ajira na vinapatikana kwa gharama ya juu zaidi na kupitia wizara tatu tofauti mfano wizara ya mambo ya ndani,wizara ya Elimu na mafunzo ya ufundi na wizara ya kazi hali inayochangia kukosa wataalamu wakati nchi nyingine zikifaidika na soko la pamoja la jumuia ya Afrika Mashariki.

Sekwaro pia ametolea mfano wa ushuru wa kodi ya forodha unaotozwa kwenye karatasi zinazoagizwa kutoka nchi mwanachama katika Jumuia ya Afrika Mashariki Kenya kuwa zipo juu sana na wakati nchi ya Uganda inatoza ushuru nafuu na kuwezesha upatikanaji rahisi wa bidhaa hiyo.
Kwa upande wake Rwechungura Mali ambaye ni Afisa Mtendaji wa chama cha wafanyabiashara mkoa wa Kagera TCCIA amesema kuwa kuna vikwazo vingi katika mpaka wa Mtukula na kuna baadhi ya watendaji wa Chakula na Dawa TFDA, Kilimo na wengineo wanafanya ubadilifu walipisha wafanyabiashara ushuru lakini hawatoi stakabadhi za malipo.

Wakichangia mjadala Afisa wa Mamlaka ya Mapato amesema kuwa wanatoza ushuru kwa kufuata mwongozo wa jumuia ya Afrika Mashariki jibu ambalo halikuweza kukidhi kiu ya wafanyabiashara na wajasrimali waliohudhuria semina hiyo.

Hata hivyo wajasriamali wametakiwa kufuata taratibu na kanuni za kuwa na vibali husika ili kuepusha kutapeliwa na kupata hasara kwa kukosa utambulisho halali wanapokuwa nchi nyingine za jumuia.

Semina ya hii imewezeshwa na mwezeshaji toka nchini Rwanda Christine Mukangoboka, wengine ni Robi Ernest Bwiru kutoka katika wizara ya Afrika ya Mashariki nchini Tanzania na wengine ni maafisa kutoka makao makuu ya jumuia ya Afrika Mashariki Arusha na wengine kutoka wizarani nchini Uganda.

JUHUDI FELIX 
0756 601054 
FADECO

Comments

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA