Nkurunziza: Sitarudi nyuma katika kugombe urais
Rais Pierre Nkurunziza wa Burundi amesema kuwa, hatasalimu amri kwa wale wanaofanya njama kutaka asigombee urais katika uchaguzi mkuu ujao nchini humo.
Hayo yamesemwa na Willy Nyamitwe, mshauri wa Rais Nkurunziza akimnukuu rais huyo ambapo pia amekosoa maandamano ya wapinzani wanaopinga azma yake ya kushiriki katika uchaguzi ujao na kuitaja hatua hiyo kuwa ni kinyume na demokrasia.
Nyamitwe amesisitiza kuwa, Rais Nkurunziza hatasalimu amri katika azma yake hiyo. Amewataja wale wanaoandamana kupinga hatua hiyo kuwa, wanatishia usalama wa wananchi katika uchaguzi ujao.
Mshauri huyo wa raia wa Burundi anasema chama tawala CNDD-FDD, kama vilivyo vyama vingine vya siasa na katika fremu ya mwenendo wa kidemokrasia, kina haki ya kumteua mgombea yeyote kimtakaye.
Kwa muda wa siku tatu sasa, maeneo kadhaa ya Burundi yamekuwa yamekumbwa na machafuko makali ambayo yamesababishwa na hatua ya chama tawala CNDD-FDD kumuidhinisha Rais Nkurunziza kupeperusha bendera ya chama hicho katika uchaguzi ujao.
Comments
Post a Comment