JIHADHARI, CHUPA YA MAJI NI HATARI
Ndicho nilichokifanya leo. Nilipuuzia ujumbe uliotumwa kwenye kundi moja (tizama picha hapo juu), nikidhani ni moja ya zile zinazotungwa ili kuwapa watu kiwewe tu, lakini baadaye nikapata wazo la kuutuma kwenye kundi jingine na kuuliza 'Inawezekanaje?"
Majibu niliyopata yamenipa sababu ya kumshukuru aliyetuma ujumbe huo kwa kunisababisha niwe makini kuhusiana na hilo. Nimefahamishwa:
Mwingine pia akachangia:
"Ni possible kabisa sis. Imeshatokea na ilimhusisha mtu namfahamu sema tu aligonga gari nyingine kwa nyuma. Chupa ya maji aliiweka kwenye ile nafasi kwenye gia pale kumbe aliposhika breki ikaanguka na hakujua so safari ikaendelea baadaye kidogo akashika breki kumbe imesogea kwenye pedal"
Mwingine pia akachangia:
"Subi hiyo ya chupa ya maji ilishanitokea mimi. Bahati nzuri nilikuwa napunguza spidi vs kusimama kabisa. I never thought chupa ya maji inaweza kusababisha."
Nimeona vyema nishirikishe na wengine hapa ili tujihadhari kabla ya ajali.
CHANZO: wavuti.com
Comments
Post a Comment