MORSI AHUKUMIWA MIAKA 20 GEREZANI

Rais wa zamani Mohammed Morsi
Rais wa zamani wa Misri Mohamed Morsi amehukumiwa kifungo cha mika 20 jela kwa kosa la kuchochea machafuko wakati wa maandamano mwezi Desemba mwaka 2012
Mohamedi Morsi alishirikishwa katika kesi hiyo pamoja na wafuasi wengine kumi na mbili wa Muslim Brothehood, ambao wamehukumiwa pia kifungo cha miaka ishirini jela.
Huu ni uamzi wa kwanza dhidi ya kiongozi wa zamani wa Misri tangu alipotimuliwa madarakani na jeshi mwezi Julai mwaka 2013
Mohamed Morsi, rais wa kwanza aliyechaguliwa chini ya misingi ya kidemokrasia nchini Misri mwezi Juni mwaka 2012 kabla ya kutimuliwa madarakani na jeshi, anaweza kukata rufaa.
Waendesha mashtaka wanamtuhumu Mohamed Morsi na viongozi wengine wa Muslim Brotherhood kuchochoea machafuko yaliyogharimu maisha ya mamia ya waandamanaji mwezi Desemba mwaka 2012.
Hisia tofauti zimetolea nchini Misri baada ya uamzi huo wa Mahakama kutangazwa. Raia wasiomuunga mkono Mohamedi Morsi wamepokea shingo upande uamzi huo. Wengi walidhani kwamba rais huyo wa zamani wa Misri angelihukumiwa adhabu ya kifo, wakibaini kwamba hukumu aliyopewa ni ndogo mno ikilinganishwa na tuhuma zinazomkabili.
Kwa upande wao, wafuasi wa Muslim Brotherhood ambao wameongea na vyombo vya habari vya kigeni na vile vinavyopeperusha kwenye mitandao mbalimbali, wamebaini kwamba kesi hiyo ni ya kisiasa, ambayo imekua ikiandaliwa na kundi la wanajeshi waliohusika katika kwa kuupindua utawala wa Morsi.

Comments

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA