MVUA YAHARIBU MAKAZI BUSEGA NA MONDULI


Simiyu

Zaidi ya wakazi 300 wa kijiji cha Lamadi Wilayani Busega mkoani Simiyu hawana sehemu za kuishi kutokana na nyumba zao kusombwa na maji kufuatia mvua kubwa iliyoambatana na upepo mkali kunyesha jana majira ya usiku.

Mvua hiyo ilisababisha mafuriko makubwa ambayo yaliyosababisha nyumba zao kuingiliwa na maji na nyingine kuezuliwa na upepo mkali baadhi yao wamehifadhiwa na ndugu na jamaa huku wengine wakikimbilia katika taasisi za serikali ikiwemo shule ya msingi Nyamajeshi iliyopo kijijini hapo.

Akizungumza katika maafa hayo diwani wa kata ya Lamadi Emanuel Desera alisema kuwa tukio hilo limetokea jana majira ya usiku baada ya mvua hiyo kunyesha kwa muda mrefu hali ambayo maji yalizidi kujaa katika maeneo ya wakazi ya watu na kusababisha nyumba nyingi kubomoka.

Desera alisema baada ya mvua hiyo kufanya uharibifu huo wananchi hao walilazimika kukimbiliakatika maeneo yaliyo salama ambapo ni shule ya msingi Nyamajashi ili kuweza kunusuru maisha yao kutokana na nyumba zao kujaa maji.

Alibainisha kuwa hali ya wananchi hao kwa hivi sasa siyo nzuri na kwani wahanga wengine wamekimbilia kwa ndugu zao kujihifadhi, huku akibainisha kuwa mafuriko bado yanaongezeka na kuiomba serikali kupeleka msaada wa chakula madawa na mahema kwa wahanga hao.

“Vitongoji vilivyokubwa na mafuriko hayo ni Kisesa, Sokoni Mwalukonge, Lukungu, Iseni B na Mwabayanda ambapo nyumba 200 zimesombwa na maji na watu zaidi ya 300 wapo katika shule ya msingi Nyamajashi ili kuweza kujinusuruna mvua,”
alisema Desera.

Mmoja wa wakazi wa jiji cha Lamadi joseph chenga ameiomba serikali kupitia ofisi ya waziri mkuu kupeleka misaada ya Mahema na Chakula ili kuawezesha wananchi hao kupata chakula kwani mpaka sasa chakula walichokuwa wakikitegemea kimesombwa na maji katika makazi yao.

Baadhi ya wananchi hao wakiongea na waandishi wa habari waliofika katika tukio hilo walisema kuwa maji hayo yamejaa kutokana na vijiji hivyo kuwa kwenye bonde hali ambayo mvua zikizidi maji hutwama na kukosa sehemu ya kuelekea hivyo yanarudi katika makazi ya watu.

”Mvua hiyo ilianza kunyesha majira ya saa sita usiku ambapo maji yalijaa katika nyumba na kusomba vitu mbalimbali pamoja na kuku hali iliyotulazimu kukimbilia katika katika shule ya msingi nyamajashi kwa ajili ya kujihifadhi,pamoja na kupata msaada zaidi kutoka serikalini,”
Alisema mmoja wa waathirika wa mafuriko.

Viongozi mbalimbali wakiwemo kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya hiyo ikiongozwa na mkuu wa polisi wa wilaya walifika eneo la tukio na kujionea uharibufu huo ikiwa pamoja na kuangalia usalama wa wananchi hao waliokumbwa na mafuriko hayo.  --- (via Simiyu News blog)


click 'VIEW WEB VERSION' below to see this video
    

Comments

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA