Taarifa: Rais Kikwete amteua Lukumay (Katibu - Rufaa za Zabuni) na Makombe (Kamishna - Udhibiti Fedha Haramu)

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Bwana Kissiok Ole Mbille Lukumay kuwa Katibu Mtendaji wa Mamlaka ya Rufaa za Zabuni za Umma.

Aidha, Rais Kikwete amemteua Bwana Onesmo Hamis Makombe kuwa Kamishna wa Kitengo cha Kudhibiti Biashara ya Fedha Haramu.

Taarifa iliyotolewa Alhamisi, mjini Dar es Salaan na Ofisi ya Katibu Mkuu Kiongozi (KMK), Balozi Ombeni Sefue, inasema kuwa uteuzi wa maofisa hao wawili ulianza Ijumaa ya Machi 27, 2015.

Kabla ya uteuzi wake, Bwana Lukumay ambaye ana diploma in Materials Managementna ni Certified Supplies Professional na pia ana MBA (Procurement and Logistics) alikuwa Ofisa Ugavi Mkuu na Kaimu Katibu Mtendaji wa Mamlaka ya Rufaa za Zabuni za Umma.

Naye Bwana Makombe kabla ya uteuzi wake alikuwa Kaimu Kamishna, Kitengo cha Kudhibiti Biashara ya Fedha Haramu. Kielimu, Bwana Makombe ana shahada za B.Com, CPA na MBA (Finance and Human Resources Management).

Imetolewa na;
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu – Dar es Salaam.

Comments

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA