MABOMU YANAVYO PIGWA UBUNGO KUTOKANA NA VURUGU KUTOKANA NA MGOMO WA MADEREVA
Jeshi la Polisi limelazimika kutumia mabomu ya machozi kuwatawanya watu wanaoleta vurugu katika kituo cha mabasi Ubungo.
Polisi Jijini Dar es Salaam wamelazimika kutumia mabomu ya machozi katika kituo cha mabasi yaendayo mikoani cha Ubungo kutuliza vurugu zinazofanywa na abiria pamoja na wananchi kufuatia mgomo wa madereva.
Shuhuda wetu ameshuhudia katika neo la Ubungo bajaji na pikipiki nazo zinalazimishwa kugoma, Dereva akileta ubishi anapigwa na usafiri wake kuharibiwa.
Mpaka sasa mabasi yanayotoka Mwanza kwenda mikoa mingine hayajaondoka kituo cha mabasi cha Nyegezi,madereva wote wamegoma baada ya serikali kuwapa miaka mitatu wawe wamekwenda shule ya udereva.
Kutoka Stendi ya Ibinzamata Shinyanga,pia hakuna gari inayoruhusiwa kutoka stendi
Umati wa abiria wakiwa kwenye kituo cha daladala cha Darajani-Ubungo huku kukiwa hakuna daladala yoyote inayofanya kazi baada ya kutokea kwa mgomo wa madereva wa Daladala jijini Dar.
Baadhi ya abiria wakiwa wamepanda magari ya mizigo baada ya kukosekana kwa daladala maeneo yote ya jiji la Dar es Salaam leo asubuhi.
Mmoja wa abiria akiongea na dereva wa kibasi kidogo kuangalia kama kuna uwezekano wa kupata usafiri maeneo ya Mwenge jijini Dar.
Katika kituo cha mabasi cha Mpakani eneo la Mwenge zilionekana Bajaj zikipakia na kushusha abiria baada ya madereva kuingia kwenye mgomo leo asubuhi.
Habari toka Morogoro zinaarifu kuwa Abiria wamejazana katika vituo vya daladala, bodaboda ndo zinatoa msaada (kwa wale wenye uwezo).
Mdau wa Malunde1 blog Kutoka Kahama anaarifu kuwa mpaka sasa hakuna basi hata moja lililotoka kwenda mikoani.
Kutoka stendi ya Mwanza pia tunaambiwa hakuna hata basi moja imeruhusiwa kutoka
Comments
Post a Comment