Miaka 5 ya Kafulila: Haya ndiyo mabadiliko ya Kigoma Kusini

SAFARI YA KIZAZI CHA KUHOJI JANA, LEO NA KESHO!

Niligombea 2010 sikuahidi kutatua kila kero na matatizo ya jimbo lakini niliahidi kuonesha tofauti ya jimbo kabla yangu na baada ya miaka mitano ya uongozi wangu.

HAYA NDIYO MABADILIKO YA KIGOMA KUSINI MIAKA MITANO

Nimepewa jimbo ukanda mzima wa ziwa hauna simu, leo kata zote ukanda wa ziwa una simu.

Nimepewa jimbo ukanda wa ziwa haupitiki kwa barabara; leo barabara zimebaki kilomita chache ifike kalya na madaraja zaidi ya 19 madogo yamejengwa.

Nimepewa jimbo kivuko cha ilagala kibovu, leo kuna kivuko bora kabisa kutoka uholanzi cha 3bilion ingawa kwenye ilani ya CCM hakikuwemo.

Nimepewa jimbo hakuna mtoto anasomeshwa, leo nimesomesha watoto 200 na wengine wamemaliza na kufaulu kuendelea.

Nimepeleka vifaa vya maabara (mobile laboratory) sekondari 17 rekodi ambayo hakuna jimbo mkoa wa kigoma limefikia hatua hiyo.

Nimepeleka vifaa vya computers, Printers, fax na photocopy machines kwa sekondari tano za ruchugi, nguruka, kalenge, sunuka na ilagala.

Nimetumia mfuko wa jimbo kuanza ujenzi wa sekondari Basanza.

Nimehakikisha kata ya Kalya inapata kituo cha Afya kwa hoja na mchango wa moja kwa moja kama njia ya kupunguza vifo vya wajawazito na watoto ukanda wa ziwa.

Nimefuta tatizo la vitanda na magodoro kituo kikubwa cha afya nguruka kwa kupeleka magodoro 20, vitanda 20 na shuka 30. Kata ya mtego, Kandaga mtandao wa simu unajengwa.

Kata ya mtego nimehakikisha inaunganishwa kwa barabara ilokuwa kero kubwa.

Nimesaidia upatikanaji wa visima vifupi kata ya mtego chagu na naendelea Mganza.

Nimehakikisha serikali imekubali kulipa mafao ya waliokuwa wafanyakaz wa mgodi wa chumvi uvinza tangu mwaka 1999.

Nimehakikisha jimbo linapata miradi mitano mikubwa ya maji rukoma, Nguruka, uvinza, kandaga na Ilagala.

Nimechangia juhudi za ujenzi kituo cha afya Kazuramimba.

Nilishawishi bank ya twiga kuleta mafunzo ya bank vijijini (VICOBA).

Nilihamasisha wajasiliamali na Halmashauri yangu ikapata trekta 10 ya mkopo kutoka JKT.

Nimepigania madai ya mapunjo ya NSSF kwa waliokuwa wafanyakaz wa mgodi wa chumvi Uvinza.

Nimetoa vifaa vya michezo kama jezi na mipira kwa timu za vijiji vyote jimbo zima. Na baadhi ya kata zimefanya ligi.

Nimepigania umeme sasa mtandao wa umeme kwa kuanzia unajengwa kuanzia ilagala, Mwakizega, Simbo, Kandaga, Kazuramimba, Uvinza na Basanza. Pia naendelea kupigania tarafa ya nguruka ipate kituo cha umeme.ukanda wa ziwa utapata umeme mpango wa REA unaofuata.

Niliahidi kuhakikisha kiwanda cha chumvi kinacha kutumia kuni kutokana na uharibifu wa mazingira. Sasa serikali ipo tayari kukifunga mpaka hapo mwekezaji atakapobadilisha teknolojia

Nimechangia makanisa na misikiti kadiri ya uwezo kwa namna mbalimbali kuliko mbunge yeyote alopata kutokea jimbo hili.

Nimehakikisha serikali inatekeleza ujenzi wa barabara mbili za lami zenye urefu wa 126km na kufanya jimbo hili kuwa na mtandao mrefu wa lami kuliko jimbo lolote mkoa wa Kigoma na ndio jimbo pekee lililopata lami 2010-2015 mkoa wa Kigoma.

Nimehakikisha serikali inajenga daraja ruchugi ambalo hata kwenye ilani ya ccm halikuwemo.

Nimehakikisha serikali inateleleza ahadi ya ujenzi wa daraja malagarasi iloshindwa tangu mwaka 1979 kwenye mpango wa kwanza wa maendeleo na hata miaka mitano ya kwanza ya utawala wa Kikwete.

Nimendelea kupinga utawala mbovu wa Mkuu wa wilaya bungeni na mpaka kushtakiwa polisi kwa kuwatetea wananchi wangu kutokana na vitendo vya Mkuu wa Wilaya kuchoma nyumba za wakulima.

Nimewapigania wananchi wangu hasa ukanda wa ziwa kwa kuitwa wakimbizi na serikali hii wakati ni raia halali. Nilipambana mbele ya waziri mkuu na kuwatoa wakazi wengi waliokamatwa mpaka kupelekwa ubalozi wa Congo lakin niliwarudishia hadhi na heshima yao kama raia. Nilipambania watu hawa ndani ya Kigoma na nje ya Kigoma kokote walipokamatwa. Niliwatoa polisi mamia ya wakazi waha kwa wabembe walioshikiliwa na polisi Dar es Salam kwa hoja za ukimbizi.

Niliahidi kujenga heshima ya jimbo letu bungeni na taifa kwa ujumla. Kupitia hoja nilotoa ya ESCROW serikali ilivunjika. (Kuivunja Serikali ndio kilele cha uwajibikaji katika vita dhidi ya mafisadi).

KAFULILA: JANA, LEO NA KESHO!

chanzo:wavuti.com

Comments

  1. Hi there! Would you mind if I share your blog with my twitter group?
    There's a lot of people that I think would really appreciate your content.
    Please let me know. Cheers

    ReplyDelete
  2. It's a pity you don't have a donate button! I'd most certainly donate to this excellent blog!
    I guess for now i'll settle for book-marking and adding your RSS feed to my
    Google account. I look forward to brand new updates and will talk about this website with my Facebook group.
    Talk soon!

    ReplyDelete

Post a Comment

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA