Rais Kikwete amteua Mgaza kuwa Balozi Saudi Arabia
- Get link
- X
- Other Apps
10 Apr 2
Hemed Iddi Mgaza |
Rais Jakaya Kikwete amemteua Hemed Iddi Mgaza kuwa Balozi wa Tanzania Saudi Arabia.
Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi (KMK), Balozi Ombeni Sefue jana imesema uteuzi huo ulianza Machi 27.
Kabla ya uteuzi huo, Mgaza alikuwa Ofisa Mambo ya Nje Mkuu, Daraja la Pili na Mkuu wa Utawala katika Ubalozi wa Tanzania Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC).
Mgaza anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Balozi Abdillah Omar ambaye mkataba wake wa utumishi umekwisha.
via gazeti la Mwananchi
- Get link
- X
- Other Apps
Comments
Post a Comment