Manyika Jr aiomba radhi Simba

IMG-20150419-WA0001
BAADA ya Simba kufungwa mabao 2-0 dhidi ya Mbeya City katika mechi ya ligi kuu soka Tanzania bara iliyopigwa uwanja wa Sokoine mwishoni mwa juma lililopita, kipa kijana wa Msimbazi, Manyika Peter Jr alilaumiwa na mashambiki kwa kudaka chini ya kiwango.
Mashabiki hawakuridhishwa na udakaji wake na kudai ameshuka kiwango tangu awe katika mahusiano ya kimapenzi na Mrembo mmoja anayeitwa Naima.
Baada ya lawama kijana Manyika Jr alikuja juu na kutoa majibu yanayoonekana pichani juu kwa mashabiki wa Simba wamamshutumu kushuka kiwango kwasababu ya mapenzi.
Baada majibu hayo ya Manyika Jr, demu wake naye akaja na maneno haya
Baada ya kuandikwa sana na kukosolewa kwa majibu yake, Manyika Jr amejitokeza na kuwaomba radhi wanasimba wake kupitia akaunti yake ya Instagram.
Huu ndio Manyika Jr ujumbe alioandika jioni ya leo
“Wanadamu wengi wanafanya makosa bila kutambua kwa kuwa na upeo mdogo wa kufikiri.Wanachama na viongozi nawaomba radhi kwa kitendo nilichokifanya kijana wenu.mnisamehe sana naahidi kutojitokeza tenah jambo hili.nawapenda sana na naipenda sana SIMBA SPORTS CLUB .Asanteni.”

Comments

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA