KWA mara nyingine twawaletea hatua za ujenzi wa mradi wa Soko la Kisasa la Mwanza (Mwanza Commercial Complex), ambao unaelekea kukamilika ikiwa sasa ni zileee hatua za finishing ukichukua miaka takribani mitatu sasa na umefikia katika hatua hii nzuri.
Mradi huu wa ujenzi wa kitenga uchumi hiki, unaendeshwa kwa ubia kati ya Halmashauri ya Jiji la Mwanza wakati Jiji hilo halijagawanywa kuwa pande mbili, na Mfuko wa Akiba kwa Watumishi wa Serikali za Mitaa (LAPF). Mradi huo unajengwa eneo la Ghana, katika Kata ya Nyamanoro iliyoko ndani ya mipaka ya Manispaa ya Ilemela.
Swali bado linabaki Jeh! Watanzania wazalendo wa nchi hii ndiyo watakao pewa kipaumbele kuwekeza biashara katika mradi huu wa mwanza Commercial Complex?
Na mradi huu, hadi utakapokamilika, unakadiriwa kugaharimu Sh bilioni 60.45.
|
Mstahiki Meya wa Jiji la Mwanza Stanslaus Mabula akitembelea soko hilo kujionea hatua za maendeleo ya ujenzi. |
|
Kwa ndani ngazi kupanda na kushuka. |
|
Engo nyingine. |
|
Parking ni ya kutosha. |
|
Ione kwa uzuri zaidi. |
|
Ni Mwanza City Commercial Complex.
chanzo:gsengo |
Comments
Post a Comment