KONGO BRAZZAVILE YAPIGA MARUFUKU UVAAJI WA HIJABU




Serikali nchini Kongo - Brazzaville imepiga marufuku uvaaji wa hijabu nchini humo.

Kwa mujibu wa taarifa iliotolewana redio ya taifa Kongo, serikali imepiga marufuku kwa waislamu kuvaa hijabu na kufunika uso, wakati wageni wakipigwa marufuku kutumia misikiti nyakati za usiku nchini kote kama sehemu ya jitihada za kupambana na ugaidi katika taifa hilo la Afrika ya Kati. 

Kwa mujibu wa Waziri wa Mambo ya Ndani, Zephirin Raymond Mboulou, uamuzi huo ulichukuliwa baada ya uchunguzi na kukamata baadhi ya watu katika vipengele vya makosa ya jinai na kudai wanaohusika na matendo hayo huvaa hijabu za kufunika uso na kuacha macho tu. 

Serekali imesema kuwa wanaruhusu kujifunika kichwa tu bila kuziba uso na wageni waotumia msikiti nyakati za usiku kama malazi wamepigwa marufuku kwani misikiti si kwa ajili ya kulala bali kwa kufanya ibada. 

Afisa wa Polisi, Mbata Ya Bakolo, ametaarifu Waislamu juu ya mwendelezo wa operesheni ya Polisi ambao una lengo la kupambana na uhalifu na uhamiaji haramu nchini Kongo.

Comments

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA