Skip to main content

Breaking News: Watu 10 wafariki dunia katika ajali ya basi Shinyanga na 51 wajeruhiwa

 

vpo
Kamanda wa jeshi la polisi mkoani Shinyanga kamishina msaidizi, Justus Kamugisha.
Na Andrew Chale wa Modewji blog
Habari zilizotufikia hivi punde katika chumba cha Modewji blog ni kuwa bado jeshi la Polisi na wasamaria wema wanaendelea kuokoa majeruhi na maiti wa ajali ya gari iliyotokea muda wa masaa mawili yaliyopita kwa kuuhusisha basi la Unique namba za usajili T148 BKK likitokea jijini Mwanza kwenda Tabora kugongana na lori katika kijiji cha Ibingo kata ya Samuye Shinyanga. 
Akizungumza na Modewji blog, Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Shinyanga, RTO Chacha Marwa alibainisha kuwa, hadi sasa ni watu 10  wamepoteza maisha huku 51, wakijeruhiwa vibaya na kuendelea kukimbizwa hospitali.
“Hadi sasa ni watu 10 wamepoteza maisha. Na tunaendelea kuokoa wengine ambao 51 ni majeruhi. hivyo bado tupo hapa kwa sasa na taarifa zaidi tutaendelea kuzitoa” aliimbi Modewji  RTO Chacha.
Hadi sasa majeruhi wamekimbizwa katika hospitali ya mkoa wa Shinyanga.
ajali
Muonekano wa eneo la ajali hiyo kwa picha iliyopigwa kwa mbali.
chanzo;mo blog

Comments

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA