FAHAMU DALILI ZA AWALI KAMA MPENZI WAKO ANAKUSALITI (ANACHEPUKA)
Wataalam wa misemo wanasema ‘ajali haina kinga’, lakini ukweli ni kwamba kuna dalili au tabia ambazo hupelekea ajali na unaweza kuzitumia kuikwepa ajali panapowezekana. Moja kati ya sababu kubwa inayovunja uhusiano kati ya wawili walioanza mapenzi kwa kula kiapo au kuahidiana mengi wakipendana sana ni ‘USALITI (MICHUPUKO)’. Na usaliti huu mara nyingi hufanywa kwa kificho sana, lakini ukiwa makini sana na uhusiano wako unaweza kuanza kugundua mapema kama mpenzi wako anakusaliti. Hizi ni dalili 5 za awali kufahamu kama mpenzi wako anachepuka…zipo dalili nyingi lakini leo tunakupa dalili zinazojikita kwenye mlengo wa MABADILIKO.. 1. ANGALIA KAMA ANA MABADILIKO YA RATIBA NA MAELEZO YA KILE ANACHOFANYA Angali kama amebadilisha ratiba ya kurudi nyumbani akiwa amechelewa sana kutoka kazini tofauti na awali, na pia maelezo yake ukiyafuatilia kwa ukaribu yanakuwa na sababu tofauti na alizowahi kukueleza kwa utaratibu wa ofisi yake awali. Angalizo: kuna wakati mabadiliko haya ya ratiba yanawez...