BAADA YA KUACHIKA ROSE NDAUKA AANGUSHA SHEREHE.
SIKU
chache baada muigizaji nyota wa filamu nchini, Rose Ndauka kutemana na
bwana wake, Malik Bandawe, Jumanne iliyopita aliangusha bonge la sherehe
iliyofana ndani ya Ukumbi wa Hoteli ya Collosseum, iliyopo Kariakoo
jijini Dar na kuhudhuriwa na mastaa kibao, Ijumaa lilikuwepo.Lakini kivutio zaidi kwenye shughuli hiyo iliyoshuhudia pia Mussa Issa ‘Cloud’ anayekaimu uongozi wa Bongo Movie Unity akiutangaza upya umoja wao, alikuwa ni shoga mkubwa wa Rose, Jacqueline Pentezel ‘Jack Chuzi’ambaye alionekana ‘akimkogesha’ fedha rafikiye wakati wa kutoa zawadi ulipowadia.
Akiwa kwenye sherehe hiyo, Rose alionekana kuwa mwenye furaha tofauti na siku chache zilizopita baada ya kukosana na mchumba wake huyo. Katika zoezi la vinywaji, baadhi ya waalikwa walikunywa hadi kulewa chakari na hivyo kuleta burudani nyingine.
Comments
Post a Comment