Mahakama ya Kisutu yamzuia Davido kuperform katika tamasha la Fiesta
Mahakama ya
Hakimu Mkazi ya Kisutu, Dar es Salaam imemzuia msanii kutoka Nigeria, Adedeji
Adelek maarufu kama ‘Davido’ kuperform katika tamasha la Fiesta linaloandaliwa
na Clouds Fm na Prime Promotion, October 18,2014.
Amri hiyo
imetolewa jana (October 17) na hakimu mkazi wa mahakama ya kisutu , mheshimiwa
D. Kisoka kufuatia maombi ya dharura yaliyowasilishwa mahakamani hapo na Times
Fm Radio na Times Fm Promotion.
Times Fm
Radio na Times Fm Promotion walipeleka maombi ya dharura mahakamani hapo
wakiitaka mahakama kumzuia msanii huyo kuperform katika tamasha hilo kwa kuwa
licha ya BASATA (Baraza La Sanaa Tanzania) kukataa kutoa kibali cha msanii huyo
kwa maelezo kuwa tayari alikuwa ameshachukuliwa kibali cha kuperform nchini
November 1 kwenye tamasha lililoandaliwa na Times Fm Radio, Clouds Fm na Prime Times Promotion
waliendelea na taratibu zote bila kujali zuio hilo la BASATA.
Times Fm
Radio na Times Fm Promotion waliiomba mahakama kuidhinisha madai yao dhidi ya
Clouds Fm, Prime Promotion na mkurugenzi wa kampuni inayomsimamia Davido, HKN
Music.
Madai hayo
ni pamoja na kulipwa fidia ya gharama na usumbufu waliosababishiwa na
walalamikiwa kadiri Mahakama itakavyoona inafaa.
Mahakama
imetoa amri kuwa msanii huyo amezuiwa kufanya onesho hilo October 18,2014 hadi
pale ufumbuzi wa kesi hiyo utakapopatikana mhakamani hapo.
Awali,
Davido alisikika katika matangazo ya Times Fm Radio akieleza kuwa atakuja
Tanzania November 1 kwa ajili ya kufanya onesho linaloandaliwa na kituo hicho
cha radio lililopewa jina la ‘The Climax’.
ORDER YA MAHAKAMA |
Comments
Post a Comment