FAHAMU DALILI ZA AWALI KAMA MPENZI WAKO ANAKUSALITI (ANACHEPUKA) ‪

Wataalam wa misemo wanasema ‘ajali haina kinga’, lakini ukweli ni kwamba kuna dalili au tabia ambazo hupelekea ajali na unaweza kuzitumia kuikwepa ajali panapowezekana.

Moja kati ya sababu kubwa inayovunja uhusiano kati ya wawili walioanza mapenzi kwa kula kiapo au kuahidiana mengi wakipendana sana ni ‘USALITI (MICHUPUKO)’. Na usaliti huu mara nyingi hufanywa kwa kificho sana, lakini ukiwa makini sana na uhusiano wako unaweza kuanza kugundua mapema kama mpenzi wako anakusaliti.

Hizi ni dalili 5 za awali kufahamu kama mpenzi wako anachepuka…zipo dalili nyingi lakini leo tunakupa dalili zinazojikita kwenye mlengo wa MABADILIKO..

1. ANGALIA KAMA ANA MABADILIKO YA RATIBA NA MAELEZO YA KILE ANACHOFANYA
Angali kama amebadilisha ratiba ya kurudi nyumbani akiwa amechelewa sana kutoka kazini tofauti na awali, na pia maelezo yake ukiyafuatilia kwa ukaribu yanakuwa na sababu tofauti na alizowahi kukueleza kwa utaratibu wa ofisi yake awali.

Angalizo: kuna wakati mabadiliko haya ya ratiba yanaweza kutokana na ukweli wa maisha na mabadiliko ya kikazi tu, hivyo unapaswa kuwa makini uonapo hili na kulichukulia kama kidokezo, kisha fuatilia taratibu.
2. ANGALIA KAMA AMEKUWA NA MABADILIKO YA ‘MOOD’, MWEPESI WA HASIRA NA KUANZISHA UGOMVI

Mpenzi anaechepuka mara nyingi huweka pembeni aibu yake, uovu wake na hasira zake na kuitafutia sababu kwako. Ataanzisha ugonvi usio na maana sanakwa lengo la kuhamishia lawama zote kwako na kukuonesha kuwa umekosea. Au mkitofautiana kidogo ata-overreact. Kwa ufupi hutafuta sehemu ya kurusha uovu wake asishitukiwe au hufanya hivyo kwa kuwa amekupunguza thamani tayari ana ameanza kupewa mwingine.

3. ANGALIA KAMA AMEPUNGUZA AU AMEACHA KABISA KUONGEA NA WEWE KAMA AWALI NA AINA YA MASIMULIZI
Jaribu kuwa makini pale unapoona mpenzi wako ameacha kuongea na wewe kama awali hasa zile stories na ucheshi alioukuwa anakupa. Unapoona ghafla hali hiyo inafifia jaribu kuwa makini. Ukaribu wenu unaweza kuwa umeanza kufifia kwa kuwa mpenzi wako amempata mtu mwingine aliyechukua sehemu yako

4. ANGALIA KAMA MPENZI WAKO ANANUKIA TOFAUTI ANAPOKUSOGELEA
Kuwa makini sana hasa pale unamsikia mpenzi wako ananukia harufu ya manukato ambayo ni tofauti kabisa na unayoyafahamu wewe awali, ama manukato ya kike ya nywele ambayo wewe hutumii. Hii inawezekana kwa kuwa hata kama alioga vizuri baada ya kumaliza kukusaliti, wakati wa kuagana wanaweza kugusana sana hivyo harufu fulani ikabaki.

Hata hivyo, anaweza kuwa akifika nyumbani anapitiliza hadi chumbani bila kukusogelea tofauti na zamani kwa kuwa hajiamini na wengine nafsi huwasuta. Hivyo unaweza kushtukia hata mtindo anaoutumia kuingia nyumbani.

5. ANGALIA KAMA AMEBADILISHA VITU ANAVYOPENDA (HOBBIES), MUZIKI, AINA YA FILAMU N.K
Inawezekana ukaanza kumuona mpenzi wako akibadili kabisa aina ya vitu alivyokuwa anapenda awali. Usiiichukulie poa, ingia ndani kwa kuwa hiyo ni ‘tabia/dalili ya ajali’ katika uhusiano wako. Anaweza kubadilia aina ya miziki anayopenda kusikiliza, filamu anazoangalia au hata vitabu anavyosoma.

Hii inaweza kutokana na kubadilishwa na aina ya mtu anayekutana nae wakati huo na kushare nae mengi. Wataaalam wa saikolojia wanasema watu huanza kubadili mtazamo na vitu wanavyopenda kwa ku-adopt tabia za watu wanaokuwa nao karibu na hasa wanaowapenda.

*Hizi ni dalili 5 tu kati ya nyingi kwa upande wa ‘MABADILIKO’, ziko dalili nyingi ambazo tutakueleza wakati mwingine. Endelea kutembelea ukurasa huu na waalike watu wengine pia. Dumisha uhusiano wako.

LIKE UKURASA WETU WA FACEBOOK KWA HABARI ZAIDI ZA MAHUSIANO https://www.facebook.com/Victoriatherapies?fref=ts

Comments

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA