AZAM TV YASAKA WAKALI WA UCHEKESHAJI, USAHILI KUFANYIKA UWANJA WA TAIFA DAR OKTOBA 10
Tanzania ni miongoni mwa nchi zilizojaa vijana wengi wenye vipaji
vikubwa katika mambo tofauti tofauti, lakini fursa ya kuonekana imekuwa
adimu sana.
Ni kawaida kabisa kupita mitaani na kuwakuta vijana wenye uwezo wa kuchekesha na kuigiza, lakini hawana kwa kwenda.
Kwa kulitambua hilo kituo bora cha Azam TV kimedhamiria kutoa fursa
kwa watu wote wanaojihisi wana vipaji vya uchekeshaji, lakini
hawajapata nafasi ya kuonekana ndani na nje ya mipaka ya Tanzania.
Katika kuhakikisa hilo, Azam TV imeandaa kipindi cha ucheshi cha
Luninga kiitwacho WASAKATONGE COMEDY SHOW na usahili kwa ajili ya
kutafuta wenye vipaji vya kuchekesha jukwaani na kuigiza vichekesho
unatarajia kufanyika ijumaa ya Oktoba 10, 2014, kuanzia saa 2:00 asubuhi
mpaka saa 12:00 jioni ndani ya uwanja wa Taifa, Dar es salaam.
Usahili huo utajali misingi ya haki na mwenye uwezo pekee ndiye
atakayepata nafasi ya kusonga mbele, hivyo kila mtu afike kujaribu
bahati yake.
Mchakato huu utaegemea zaidi katika kigezo cha Ubunifu kwa minajili
ya kuchekesha, kuwa mwepesi katika ucheshi, kuwa na mawazo ya haraka
katika ucheshi na jinsi gani anaweza kushirikiana na wenzako kama timu
moja.
Kwa mshiriki yeyote yule kutoka nje ya mkoa wa Dar es salaam bado
ana nafasi ya kushiriki usahili isipokuwa gharama zote zitakuwa juu
yake.
Ili kutengeneza timu ya WASAKATONGE mchakato utakuwa wa awamu mbili;-
Mosi; kutakuwa na usahili wa wazi utakaofanyika uwanja wa ndani wa
taifa (Indoor); kwa wale wachache watakaopita kulingana na hitaji la
kamati watapewa utaratibu juu ya kipi kitakachoendelea kwa mzunguko wa
pili.
Pili; kutakuwa na mchujo utakaopelekea kuchaguliwa kwa watu
wachache, wasiozidi kumi na hao ndio watakaotengenezwa kwa kupatiwa
mafunzo ili kuwa wachekeshaji/waigizaji. Watakaobahatika watakuwa
WASAKATONGE wa Azam tv.
Mambo ya Zingatia!!!
Usaili huu ni wa wazi, Wasahiliwa watapaswa kujigharamia usafiri na
chakula, Hakuna zawadi kwa washindi. Mafunzo ya uchekeshaji yatatolewa
kwa washindi 10
Comments
Post a Comment