MWANAMKE ATAJWA MAUAJI YA PROF CHUO KIKUU


Stori: Makongoro Oging’ na Haruni Sanchawa

MAUAJI ya aliyewahi kuwa Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Profesa Athuman Juma Livigha (63) yaliyotokea nyumbani kwake, Bunju ‘B’, Septemba 30, mwaka huu kwa kupigwa risasi na watu wasiojulikana yameibua mengine ambapo sasa baadhi ya ndugu wamemtaja mwanamke mmoja kuwa huenda anahusika.
Profesa Athuman Juma Livigha enzi za uhai wake.
Wakizungumza na Uwazi siku ya mazishi ya profesa huyo wiki iliyopita, ndugu hao bila kutaka jina la mwanamke huyo walisema kwa asilimia kubwa mwanamke huyo aliyekuwa haelewani na marehemu anatakiwa kufuatiliwa vizuri nyendo zake.
“Huyo mwanamke alikuwa karibu sana na marehemu lakini ghafla akapotea, akawa haonekani na tukasikia  yupo tu hapa Dar. Kinachotushangaza hata katika msiba wa profesa hajafika.
“Ni kwa nini kipindi hiki awe muoga wa kuja wakati anafahamika na sisi wanafamilia tunamjua?” alihoji mmoja wa wana ndugu hao ambaye hakuwa tayari kutaja jina lake.
Mwili wa Profesa Athuman Juma Livigha ukiswaliwa kwa ajili ya mazishi.
Kwa mujibu wa majirani wa marehemu,  siku ya tukio walisikia mlio wa risasi mara moja na sauti ya marehemu ikisema uwiii baadaye kukawa kimya, ndipo kesho yake mwili wake ukaonwa na mfanyakazi wake anayetunza bustani ambaye anaishi jirani na nyumbani kwa marehemu.
Uchunguzi wa Uwazi ulionesha kuwa, siku ya tukio marehemu alifika nyumbani kwake saa tatu usiku na kuegesha gari ndani kisha aliingia ndani na kuwasha taa za ndani na nje.Baadaye marehemu alitoka nje kwa lengo la kuchukua mizigo ndani ya gari, ndipo wakati anaingia watu wasiojulikana walimpiga risasi akiwa mlangoni.
Mwili wa Profesa Athuman Juma Livigha ukipelekwa makaburini kwa ajili ya mazishi.

Ilibainika kuwa baada ya kupigwa risasi, alijitahidi kukimbia ili kujiokoa lakini aliishiwa nguvu akadondoka chini na wauaji walimchukua na kumlaza barabarani karibu na kwake kisha kumfunika kwa kanga.
Marehemu Profesa Livigha alizikwa Alhamisi iliyopita kwenye Makaburi ya Bunju ‘B’ jijini Dar es Salaam.
Mungu ailaze pema peponi roho yake. Amina.\


Chanzo: globalpublishers

Comments

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA