BWANA HARUSI AINGIA MITINI NDOA YABUMA
Tukio
hilo la aina yake lilijiri maeneo ya Kitunda-Kati jijini Dar, wiki
iliyopita ambapo chanzo makini kiliwajulisha Oparesheni Fichua Maovu
(OFM) ya Global Publishers kwamba, kuna ndoa ya mtoto inafungwa kinyume
cha sheria.
Baada ya kunyetishiwa ishu hiyo, OFM walitinga kwenye sherehe hiyo na kuanza kuwahoji baadhi ya ndugu ambao walikiri kwamba kweli ile ilikuwa ni ndoa ya mtoto aliyeacha shule akiwa kidato cha pili.
Akizungumza na OFM, Husna alisema aliamua kuolewa kwa sababu aliacha shule kutokana na kukosa ada.

Husna akilia baada ya ndoa kubatilika.
Alisema kwamba, darasani alikuwa haelewi chochote alichokuwa
akifundishwa hivyo hakuwa na kazi yoyote.“Baba na mama yangu wameachana
siku nyingi, sasa nilikuwa nalipiwa ada na mama huku kipato chake kikiwa
ni kidogo.
“Niliamua kuachana na shule maana nilikuwa sielewi chochote kwa
sababu niliugua mapepo, nimeamua mwenyewe kuolewa jamani maana sina kazi
ya kufanya,” alisema Husna.Baada ya baadhi ya watu kuwashtukia OFM,
walimpa taarifa bwanaharusi kwa simu na hakuonekana na ndoa hiyo
ikaishia hewani kwani jamaa huyo hakufika kwa kuhofia hilo.
Baadhi ya ndugu wa bwanaharusi walikuja juu na kutaka warudishiwe
mahari yao lakini mjomba wa mtoto huyo aliwasihi kwamba watakaa kama
familia na watazungumza na wako tayari kurudisha mahari.
Baada ya ndoa hiyo kubuma, mtoto Husna aliangua kilio huku akisema kwamba anampenda huyo mchumba’ke huku mama yake naye akiangua kilio akidai anaumia kwani hajui atakapozitoa hizo fedha za mahari shilingi laki nne kwani kipato chake ni kidogo.

chanzo:globalpublishers
Comments
Post a Comment