STARS YAICHAPA 4-1 BENIN
Thomas Ulimwengu akikwaana na beki wa Benin (jezi nyeupe).
Kipa wa Benin, Farnoue Fabien akijaribu kuokoa mpira wa kichwa uliopigwa na Nadir Haoroub 'Cannavaro' bila mafanikio.
Nadir Haoroub 'Cannavaro' (kushoto) akishangilia baada ya kuipatia Stars bao la kwanza. Kulia ni Oscar Joshua.(P.T)
Waziri
Mkuu Mizengo Pinda, Rais wa TFF, Jamal Malinzi na Mkuu wa Mkoa wa Dar es
Salaam, Said Mecky Sadick wakifuatilia mechi hiyo.
Amri Kiemba (wa pili kushoto) akipongezwa na wenzake baada ya kuifungia Stars bao la pili.
Mashabiki wa Stars wakifurahia ushindi.
KIKOSI
cha Taifa Stars leo kimewapa raha mashabiki baada ya kuishushia kichapo
cha mabao 4-1 timu ya Taifa ya Benin kwenye mechi ya kirafiki
iliyochezwa Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Katika mechi hiyo, mgeni rasmi alikuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mizengo Pinda.
Mabao
mawili ya Stars yamefungwa kipindi cha kwanza na Nadir Haoroub
'Cannavaro' dakika ya 16 ya mchezo akiunganisha mpira kwa kichwa huku
bao la pili likiwekwa kimiani na Amri Kiemba Ramadhan katika dakika ya
40. Mpaka mapumziko Stars walikuwa mbele kwa mabao 2-0.
Thomas
Ulimwengu aliiandikia Stars bao la tatu dakika ya 49 ya kipindi cha pili
baada ya kupokoea krosi safi kutoka kwa Mrisho Ngasa.
Juma
Luizio aliifungia Stars bao la nne kwenye dakika ya 71 na kufanya
matokeo kuwa 4-0 kabla ya Benin kupata bao lao la kufutia machozi
kupitia kwa Suano Fadel dakika ya 92 ya mchezo. Mpaka mwisho wa mchezo,
Stars 4-1 Benin.
(PICHA NA RICHARD BUKOS / GPL)
Comments
Post a Comment