LORRAINE ATUA NCHINI APONGEZA WATANZANIA
Lorraine Clement akipungia
watu waliofika kumlaki , alipokuwa akiwasili uwanja wa ndege JNI,
alipokuwa akitokea nchini, Thailand, kushiriki mashindano ya Miss Grand
International 2014, ambapo Lorraine aliibuka nafasi ya 20 bora.
Na Andrerw Chale
MWANADADA Lorraine Clement
aliyeiwakilisha Tanzania katika mashindano ya urembo ya kimataifa ya
Miss Grand International 2014, na kufanikiwa kushika nafasi ya 20 bora
katika shindano lililofanyika mjini, Bangkok, Thailand, ametua nchini
jana Oktoba 9 majira ya saa 10 jioni na kuwashukuru watanzania kwa
kumuunga mkono.
Akizungumza na wandishi wa habari
muda mfupi alipowasili uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere,
Jijini Dar es Salaam, Lorraine aliwashukuru wadau mbalimbali kwa
kufanikisha ushiriki wake kwenye mashindano hayo makubwa duniani,
ikiwemo kampuni ya Redline Communication Ltd, Iliyofanikisha mshiriki
huyo kushiriki kwa mwaka huu.
“Pongezi kwa wadau wote
mliofanikisha mimi kupeperusha vyema bendera ya Tanzania. Millen
Magese kupitia kampuni yake ya MMG, Jacqueline Kibacha, Doreen
Mashika, Husna Tandika na wengine wengi.
Lorraine Clement akishukuru
Mungu, alipokuwa akiwasili uwanja wa ndege JNI, alipokuwa akitokea
nchini, Thailand, kushiriki mashindano ya Miss Grand International 2014,
ambapo Lorraine aliibuka nafasi ya 20 bora.
Katika mapokezi hayo, Lorraine
alilakiwa pia na wazazi wake pamoja na mtendaji Mkuu wa Redline
Communication, Abubakar Faraji ‘Abu’ na wadau wengine walijitokeza
uwanjani hapo.
Kwa upande wake, Mama Mzazi wa
Lorraine, Paula David aliwashukuru watanzania kwa kumpigia kura mwanae
na kupeperusha vyema bendera ya Tanzania.
Hii ni kwa mara kwanza, mtanzania
huyo anashiriki shindano hilo ambalo kwa hapa nchini linaendeshwa na
kampuni ya Redline Communication Ltd, ambapo mshiriki wake huitwa
‘Miss Grand Tanzania’, kwa mwaka huu, Lorraine alikuwa ni mshindi wa
pili kwenye shindano la Tanzania Top Models 2013.
Aidha, Katika shindano hilo,
mwanadada, Daryanne Lees kutoka nchi ya Cuba, ndiye aliyetwaa taji hilo
kwa mwaka huu. Wengine ni Miss Ethiopia, Hiwot Mamo na Miss Canada,
Kathryn Kohut.
Shindano hilo la Miss Grand
International, kwa sasa ni msimu wa pili likifanyika nchini Thailand,
tokea kuanzisha mwaka 2013. Mshindi wa mwaka huu, ameweza kunyakua
kitita taslimu cha dola za kimarekani 40,000, pamoja na thamani za
ndani.
Lorraine akilakiwa na meneja wake Abubakar Faraji.
Lorrainea kiwa na familia yake na mama yake (kulia).
chanzo:fullshangwe.
Comments
Post a Comment