AFISA KAZI II ( LABOUR OFFICER II) – NAFASI 21

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
OFISI YA RAIS
SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA
UMMA
Kumb. Na EA.7/96/01/H/11            16 Oktoba, 2014
 

TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI
Sekretariati ya Ajira katika Utumishi wa Umma ni chombo ambacho kimeundwa kwa
mujibu wa Sheria ya Utumishi wa Umma Na. 8 ya mwaka 2002 kama ilivyorekebishwa
na Sheria Na. 18 ya mwaka 2007 kifungu 29(1). Kwa mujibu wa Sheria hiyo, chombo
hiki pamoja na kazi zingine kimepewa jukumu la kutangaza nafasi wazi za kazi
zinazotokea katika Utumishi wa Umma kwa niaba ya Waajiri (Taasisi za Umma).
Katibu wa Sekretarieti ya Ajira Katika Utumishi wa Umma anakaribisha maombi ya
Watanzania wenye sifa na uwezo wa kujaza Nafasi za kazi 21 kwa ajili ya Katibu Mkuu
Wizara ya Kazi na Ajira.
NB: MASHARITI YA JUMLA KWA KAZI ZOTE.
Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania na wenye umri usiozidi miaka 45
i.  Waombaji wote waambatishe cheti cha kuzaliwa.
ii.  Waombaji ambao tayari ni watumishi wa Umma na wamejipatia sifa za kuingilia
katika kada tofauti na walizonazo, wapitishe barua zao za maombi ya nafasi za
kazi kwa waajiri wao na Waajiri wajiridhishe ipasavyo.
iii.  Nafasi  ya  kazi  inayoombwa  iandikwe  juu  ya  bahasha,  kutozingatiwa  hili
kutasababisha maombi ya kazi kuwa batili.
iv.  Waombaji  waambatishe  maelezo  binafsi  yanayojitosheleza  (Detailed  C.V)  yenye
anwani na namba za simu za kuaminika pamoja na majina ya wadhamini (referees)
watatu wa kuaminika.
v.  Maombi    yote    yaambatane  na  vyeti  vya  taaluma,  maelezo,  nakala  za  vyeti  vya
kidato  cha  nne  na  kidato  cha  sita kwa wale  waliofikia  kiwango  hicho  na  vyeti  vya
2
kuhitimu  mafunzo  mbalimbali  kwa  kuzingatia  sifa  za  kazi  husika.  Viambatanisho
hivyo vibanwe sawa sawa kuondoa uwezekano wa kudondoka au kupotea.
-  Postgraduate/Degree/Advanced Diploma/Diploma/Certificates.
-  Cheti cha mtihani wa kidato cha IV na VI
-  Computer Certificate
-  Vyeti vya kitaaluma (Professional certificates from respective boards)
-  Picha moja “Passport size” ya hivi karibuni iandikwe jina kwa nyuma.
vi.  Testmonials”,  “Provisional  Results”,  “Statement  of  results”,  hati  matokeo  za
kidato  cha  nne  na  sita  (FORM  IV  AND  FORM  VI  RESULTS  SLIPS)
HAVITAKUBALIWA.
vii.  Waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na
kuidhinishwa na Mamlaka husika (TCU na NECTA).
viii.  Waombaji  waliostaafishwa  katika  Utumishi  wa  Umma  hawaruhusiwi  kuomba
isipokuwa kama wanakibali cha Katibu Mkuu Kiongozi.
ix.  Waombaji  kazi  ambao  tayari  ni  waajiriwa  katika  nafasi  za  kuingilia  walioko
katika  utumishi  wa  umma  wasiombe  na  wanatakiwa  kuzingatia  maelekezo
yaliyo katika Waraka Na CAC. 45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba 2010.
x.  Uwasilishaji  wa  taarifa  na  sifa  za  kugushi  wahusika  watachukuliwa  hatua  za
kisheria.
xi.  Mwisho wa kupokea barua za maombi ni tarehe 31 Oktoba, 2014
xii.  Aidha,  uwasilishaji  wa  barua  kwa  mkono  katika  ofisi  za  Sekretarieti  ya ajira
HAURUHUSIWI.
xiii.  Maombi  yanaweza  kuandikwa  kwa  Lugha  ya  Kiswahili  au  Kiingereza  na  yatumwe
kupitia posta kwa anuani ifuatayo.


 

Katibu,                    AU                   Secretary,
Sekretariati ya Ajira katika             Public Service Recruitment
Utumishi wa Umma,                        Secretariat,
SLP.63100,                                       P.O.Box 63100
Dar es Salaam.                                  Dar es Salaam.

1.1  AFISA KAZI II ( LABOUR OFFICER II) – NAFASI 21

Nafasi hizi ni kwa ajili ya Wizara ya Kazi na Ajira
1.1.1  MAJUKUMU YA KAZI
·  Kupokea na kuchambua malalamiko mbalimbali yanayohusu Sheria za kazi
·  Kufanya Ukaguzi wa Utekelezaji wa Sheria za Kazi.
·  Kukusanya taarifa na takwimu za kazi kutoka sehemu za kazi.
·  Kupokea na kuchambua taarifa za migogoro ya kazi.
·  Kupokea na kuchambua maombi ya kuandikisha mikataba ya hiari.
·  Kupokea na kuchambua madai ya fidia na kiinua mgongo
·  Kuandikisha watafuta kazi (job Seekers)
·  Kupokea na kuandikisha nafasi za kazi toka kwa waajiri.
·  Kupokea  na  kuchambua  maombi  ya  vibali  vya  ajira  ya  wageni  na  kutunza
kumbukumbu za ajira za wageni nchini
·  Kukusanya  taarifa na  takwimu  zinazohitajika  kwa  ajili   ya  kamusi  ya  Kazi
(Dictionary of Occupational Titles )


1.1.2  SIFA ZA MWOMBAJI
·  Kuajiriwa wenye Shahada ya Sheria au Sayansi ya Jamii (Sociology)
1.1.3  MSHAHARA
Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS D kwa mwezi
 

X.M. DAUDI
Katibu
Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma

Comments

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA