Maneno ya bango hili la Walimu ndiyo yalisababisha Polisi walirukie

(picha: Gazeti la Mwananchi)

Maandamano ya walimu kuingia katika Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba kuadhimisha Siku ya Walimu Duniani, juzi yalipata mtafaruku baada ya polisi kuyaingilia na kuchana bango mojawapo lililohoji posho za wajumbe wa Bunge la Katiba.
Bango hilo la kitambaa cheupe lilikuwa na maandishi yanayohoji posho ya Sh300,000 (Sh230,000 kama posho ya kujikimu na Sh70,000 ambazo ni posho ya vikao) waliyokuwa wanapata wajumbe wa Bunge la Katiba, yakilinganishwa na kazi kubwa wanayofanya walimu.

Ujumbe wenyewe ulisomeka hivi:
“Haki iko wapi? Usawa uko wapi? Posho ya Mjumbe Bunge la Katiba Tsh 300,000/= mshahara wa Mwalimu Tsh 370,000/= kwa mwezi. No big results without big salary”.

Hata hivyo bango hilo lilichanwa hatua chache kabla ya walimu hao hawajaingia uwanjani humo, ambapo mgeni rasmi alikuwa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda.


Mwenyekiti wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT), mkoani Kagera Dauda Bilikesi, alisema amesikia habari za bango hilo kuharibiwa lakini akasema asingezungumza kwa kina kuhusu suala hilo kwa kuwa hayo yamepita.

Comments

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA