KIFO CHA MWALIMU BAADA YA MATESO-4

Jijini Dar es Saalam, Waziri Mkuu Frederick Sumaye, alifanya kikao na viongozi mbalimbali wa serikali nyumbani kwake Oysterbay, kujaribu kutafuta njia za kupata hela za kugharimia mazishi ya Mwalimu ambayo nchi 61 zilithibitisha kuhudhuria.
Ghadafi, Moi kuhudhuria mazishi

Rais Muamar Ghadafi wa Libya, Daniel Arap Moi wa Kenya na Yoweri Museveni wa Uganda ni miongoni mwa marais wengi waliosema wangehudhuria mazishi ya Mwalimu Nyerere.

Wengine ni pamoja na Prince Clans wa Uholanzi, Waziri Charles Josselin muwakilishi kutoka Ufaransa, Waziri Hon Zedhong muwakilishi wa rais wa China, Waziri Jan Trojborg muwakilishi wa serikali ya Denmark, Grace Machel aliyekuwa mke wa rais wa zamani wa Msumbiji na Nelson Mandela wa Afrika Kusini. Pia Katibu Mkuu wa OAU, Dk. Salim Ahmed Salim.
Katika…

Katika hali isiyo ya kawaida, daktari aliyemtibu Mwalimu hadi kuyafikia mauti yake, alitangaza kusamehe malipo yote ya kazi yake kwa Mwalimu kama ni mchango wake kwa familia ya Mwalimu na taifa letu kwa ujumla. Msemaji wa familia ya Mwalimu, Joseph Butiku, ndiye aliyetoa taarifa hizo zilizoandikwa na magazeti nchini.

Profesa David Mwakyusa alikuwa daktari wa Baba wa Taifa tangu mwaka 1987 hadi Oktoba 14, 1999, siku Mwalimu alipofikwa na mauti jijini London, Uingereza kutokana na ugonjwa huo wa saratani ya damu (leukemia).

Katika mahojiano aliyopata kufanya muda mfupi baada ya kifo cha Mwalimu, Profesa Mwakyusa alisema walimjulisha Mwalimu kila kitu kuhusu ugonjwa wa leukemia.

Hata hivyo, kwenye maelezo yake anathibitisha namna ugonjwa huo ulivyobadilika ghafla na kumsababishia mauti, ilhali kila alipopimwa ilionekana hakuwa na sababu za kuanza matibabu mapema.

Alisema Mwalimu alikuwa mtu mwenye afya nzuri kwa ujumla, ukiacha matatizo madogo madogo.

Itaendelea wiki ijayo.

chanzo:globalpublishers

Comments

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA