Halima Mdee apelekwa korokoroni Segerea


Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (BAWACHA) ambaye pia ni Mbunge wa Kawe, Halima Mdee akitoka katika chumba cha Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam kulekea katika Gereza la Segerea baada
ya kukosa dhamana katika kesi inayoamkabili pamoja na wanachama wenzake ya kuandamana bila kibali cha polisi na hivyo kushindwa kutii amri halali ya Jeshi la Polisi la kutofanya maandamano.

Halima Mdee akielekea kupanda gari la Polisi kuelekea Gereza la Segerea huku akiwa chini ya ulinzi wa Polisi.


Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake wa Chadema (Bawacha), Halima Mdee akipanda gari la Polisi kuelekea Gereza la Segerea, baada kukosa dhamana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam. 


Baadhi ya wanachama na wafuasi wa CHADEMA waliofika Mahakamani hapo kusikiliza kesi hiyo wakipaza sauti zao.

Picha na maelezo: Francis Dande via Habari Mseto blog.

Comments

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA