MGONJWA WA KWANZA WA EBOLA MAREKANI AFARIKI

Mtu wa kwanza kupatikana na ugonjwa wa Ebola nchini Marekani amefariki ,hayo ni kwa mujibu wa maafisa wa afya katika hospitali ya Texas.

Thomas Eric Duncan aliyeambukizwa ugonjwa wa Ebola huko nchini Liberia ,alikuwa amewekwa katika karantini katika hospitali moja ya mjini Dallas ili kupewa dawa za majaribio.
Awali ,Marekani ilitangaza masharti mapya ya usalama katika viingilio vyote vya taifa hilo ili kuwakagua wasafiri walio na dalili za ugonjwa huo.

Zaidi ya watu 3000 wamefariki na wengine 7500 kuambukizwa wengi wao kutoka Afrika Magharibi katika mlipuko mbaya wa ugonjwa wa Ebola.

Huku Dancun akiwa raia wa kwanza nchini Marekani kupatikana na ugonjwa huo,raia watatu wa Marekani pamoja na mpiga picha mmoja waliambukizwa virusi vya ugonjwa huo nchini Liberia.
Habari hizo zilijiri mda mchache tu baada ya waziri wa maswala ya kigeni nchini Marekani John Kerry kutoa wito kwa mataifa yote kuimarisha juhudi zao za kukabiliana na ugonjwa huo.

Chanzo: BBC swahili.

Usisahau click matangazo mbalimbali unayoyaona katika blog hii mpenzi msomaji.

Comments

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA