VIDEO:JAJI LUBUVA ATANGAZA NEC KUAHIRISHA ZOEZI LA KURA YA MAONI

02 Apr 2


Tume ya Taifa ya Uchaguzi, NEC imetangaza kusogezwa mbele upigaji kura ya maoni iliyokuwa ifanyike tarehe 30 mwezi huu mpaka hapo zoezi la kuandikisha wananchi wote katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura litakapokamilika.

Tangazo hilo limetolewa leo na Mwenyekiti wa NEC, Jaji Damian Lubuva mbele ya wanahabari jijini Dar es Salaam akisema kuwa ni lazima wananchi wawe wameandikishwa katika daftari hilo, shughuli inayotarajiwa kukamilika mwezi Julai mwaka huu, ndipo waweze kupiga kura. Amesema tarehe mpya ya zoezi hilo litatangazwa hapo baadaye baada ya kushauriana na Tume ya Uchaguzi Zanzibar.



Comments

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA