KATIBU MKUU WA UMOJA WA MATAIFA ASISITIZA KUWA ISRAEL NI UTAWALA WA KIBAGUZI
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa asisitiza kuwa Israel ni
utawala wa kibaguzi
Kwa kuzingatia kuwa utawala wa Kizayuni wa Israel
unatambuliwa kuwa moja ya nembo za ubaguzi katika uga wa kimataifa, ukweli ni
kuwa hata viongozi wa Umoja wa Mataifa pia wamekiri kuhusiana na suala hilo
kutokana na miamala ya kibaguzi inayotekelezwa na utawala huo.
Katika uwanja huo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amesema
kuwa Israel inatekeleza siasa za kuangamiza kizazi huko Quds inayokaliwa kwa
mabavu.
Ban Ki-moon amesema katika ujumbe wake uliosomwa jana na
mjumbe wake kwenye "Mkutano wa Kimataifa wa Quds" huko Jakarta mji
mkuu wa Indonesia kwamba sababu inayowatia hasira Wapalestina katika ardhi za
zinazokaliwa kwa mabavu ni ukaliaji mabavu wa Israel pekee.
Ujumbe huo umebainisha kuwa, mwaka 1967 Israel
ililiunganisha eneo la Baitul Muqaddas ya Mashariki na maeneo mengine
iliyoyaghusubu na sasa inajaribu kuendeleza siasa zake hizo ili kuyaweka chini
ya udhibiti wake maeneo mengine zaidi ya Baitul Muqaddas na kupunguza idadi ya
wakazi wa Kipalestina katika maeneo hayo.
Ujumbe wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa vilevile
umesisitiza kuwa Israel inatekeleza siasa za kuangamiza kizazi huko Baitul
Muqaddas; huku ikiwafukuza raia wa Kipalestina majumbani mwao. Ban Ki-moon kwa
mara nyingine tena amesisitiza kuwa kwa mtazamo wa Umoja wa Mataifa ni kuwa
ujenzi wa vitongoji vya walowezi wa Kiyahudi unaofanywa na Israel ni kinyume
cha sheria na unakinzana na sheria za kimataifa.
Hakuna shaka kuwa ubaguzi wa hali ya juu wa utawala wa
Kizayuni unadhihirisha ni kwa kiwango gani jamii ya kimataifa inavyokabiliwa na
utawala ambao ni mbaya zaidi kuliko utawala wa ubaguzi wa rangi wa Apartheid na
ufashisti.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ametoa radiamali yake kwa
vitendo vya ukandamizaji na kidhulma vya utawala wa Kizayuni wa Israel katika
hali ambayo utawala huo unaendelea kushadidisha miamala yake mibovu na misimamo
ya uhasama na kibaguzi dhidi ya Wapalestina; jambo linaloitia wasiwasi jamii ya
kimataifa.
Kuongezeka jinai na kuuawa kila uchao raia wa Palestina
wasio na hatia khususan katika wiki za hivi karibuni ambapo hadi sasa
Wapalestina 125 wameuawa shahidi na wanajeshi wa Israel, kunatokana na utawala
huo kuwa na mizizi na asili ya mitazamo ya kibaguzi.
Siasa za kibaguzi na
maangamizi ya kizazi yanayofanywa na utawala wa Kizayuni yanadhihirisha namna
utawala huo unavyojishughulisha zaidi na kutenda jinai na kukiuka haki za
mataifa na kaumu mbalimbali, kama ilivyokuwa katika zama za Wanazi huko
Ujerumani, Mafashisti huko Italia, na mfumo wa ubaguzi wa rangi yaani
(Apartheid) nchini Afrika Kusini.
Miamala isiyo ya kibinadamu inayotekelezwa na
utawala wa Kizayuni wa Israel imeitia wasiwasi jamii ya kimataifa na
itakumbukwa kuwa mwaka 1975 Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa pia lilitoa azimio
nambari 3379 na kuutaja utawala wa Kizayuni kuwa ni sawa na utawala wa
kibaguzi, kufuatia malalamiko ya jamii ya kimataifa dhidi ya utawala huo
ghasibu.
Japokuwa azimio
hilo lilifutwa kati kati ya muongo wa 90 kufuatia mashinikizo ya serikali za
Magharibi na baada ya kuathiriwa na madai ya uwongo ya utawala wa Kizayuni
kwamba inataka amani, lakini utendaji wa utawala wa Kizayuni umeonyesha utawala
huo haujapunguza hata chembe siasa zake hizo za kibaguzi bali umezishadisisha;
na huu ni uhakika wa mambo ambao ameukiri wazi Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa
kuhusu Israel.
Hii ni katika hali ambayo kamati ya kupambana na ubaguzi
ya Umoja wa Mataifa pia hivi karibuni ilibainisha wasiwasi wake kuhusu hatua ya
Israel ya kupuuza sheria za kimataifa na kutoheshimu haki za binadamu na
kutahadharisha kuhusu hali mbaya waliyonayo raia wa Kipalestina katika ardhi
zinazokaliwa kwa mabavu. Kamati hiyo imesisitiza kuwa utawala wa Kizayuni
unapasa kusailiwa.
Comments
Post a Comment