Watu 14 wauawa kwa risasi Marekani
Polisi wenye silaha wakipiga doria katika eneo palipotokea mauaji hayo.
Polisi
nchini Marekani imesema takriban watu 14 wameuawa na wengine 14
kujeruhiwa baada ya kupigwa risasi na watu wenye silaha katika mji wa
San Bernadino mashariki mwa Los Angeles.
Polisi
mjini humo inasema tukio hilo imetokea kwenye kituo cha huduma kwa watu
wenye ulemavu na inawezekana lilihusisha watu watatu wenye silaha ambao
wametoroka kwa gari.
Watu hao wenye silaha wanasemakana walivyalia kijeshi na walitumia silaha za masafa marefu.
Mkuu wa
kituo hicho cha watu wenye ulemavu palipoteka mauaji hayo ya kinyama
anasema milio ya silaha ilisikika katika jengo lililokodishwa kwa ajili
ya pati iliyoandaliwa na Idara ya Afya.
Mmoja ya ndugu wa wafiwa akifarijiwa.
Rais wa
Marekani Barack Obama amelaani shambulizi hilo na kusema Marekani
imekumbwa na tukio la mauaji ya watu wengi ambalo halifanani na jingine
lolote duniani.
Kwa
upande wake Mkurugenzi Msaidizi wa Shirika la kijasusi la FBI David
Bowdich anasema sababu kubwa ya mauaji hadi haijafahamika.
"Kwa
wakati huu ninaelewa moja ya maswahili yenu ni kuhusu tukio hili la
kigaidi. Ninawaeleza sasa kuwa hatujui kama hili ni tukio la kigaidi kwa
hiyo tunaanzia mwanzo kufanya kazi na wenzetu waliopo katika eneo hili.
Tunadhani inaweza kuwa, pia inaweza isiwe lakini tunafanya kazi bega
kwa bega nao kuanzia mwanzo. Kama mambo yatabadilika tupo hapa na hakuna
hatua yoyote itakayopotea wakati uchunguzi utakapokuwa unaendelea."
Alisema.BBC
Comments
Post a Comment