Iran yakana uhusiano na magaidi
Raia wa Iran
Serikali
ya Iran imekana kuwa na uhusiano wowote na wanaume wawili waliokamatwa
wakikisiwa kupanga mashambulizi ya kigaidi dhidi ya maeneo
yanayomilikiwa na mataifa ya magharibi nchini kenya.
Balozi wa
Iran nchini Kenya Hadi Farajvad, anasema kuwa licha ya kuwepo uwezekano
kuwa wanaume hao walizuru Iran, hakuna aliye na uhusiano na mashirika
ya usalama ya nchi hiyo.
Siku ya
Jumamosi taarifa kutoka kwa wizara ya mambo ya ndani nchini kenya,
ilisema kuwa wanaume hao walikiri kuwa walikuwa na njama ya kupanga
mashambulizi ya kigaidi dhidi ya maeneo yanayomilikiwa na mataifa ya
magharibi nchini Kenya, na walikuwa na uhusiano na kikosi cha kijeshi
kinachofahamika kama Quds Force nchini Iran.BBC
Comments
Post a Comment