MBWANA SAMATTA APONGEZWA KWA KUJIUNGA NA KLABU YA GENK YA UBELGIJI
Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape Nnauye(kushoto) akiongea na Mchezaji wa Timu ya TP Mazembe Mbwana Samatta(kulia) leo jijini Dar es salaam.Mbwana amemtembelea waziri Nape ofisini kwake na kuomba baraka za wizara katika kinyanganyiro cha kugombea uchezaji bora wa afrika anayechezea ligi za ndani na pia kumpa habari njema za yeye kutegemea kujiunga na timu ya Ubelgiji ya Genk.
Mchezaji wa TP Mazembe Mbwana Samatta(wa kwanza kushoto)akiongea na waandishi wa habari(hawapo pichani) sababu za yeye kumtembelea Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo katika ofisi ya Wizara hiyo.Mbwana alisema kuwa amemtembelea waziri uyo kwa ajili ya kumfahamisha kuwa yumo katika kinyanganyiro cha kugombea uchezaji bora wa afrika anayechezea ligi za ndani na hivyo kuomba baraka za Wizara.Pia kumpongeza Mhe. Nape kwa kuchaguliwa kuwa waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo.Mbwana anategemea kujiunga na klabu ya Mpira ya Genk ya Ubelgiji kwa mkataba wa miaka minne.
Waziri wa Habari,Utamaduni,sanaa na Michezo Mhe.Nape Nnauye(katikati)akiongea na waandishi wa Habari na kuwaomba watanzania kumwombea Mbwana Samatta ili ashinde katika kinyanganyiro cha kugombea uchezaji bora wa afrika anayechezea ligi za ndani kwani ni jambo la Taifa zima.Mhe Nape pia alimhakikishia kuwa Serikali ipo nyuma yake na ipo katika mkakati wa kuifanya michezo kuwa Shughuli Rasmi kwani itawafaidisha wanamichezo na Serikali kwa kupata kodi. Picha na Daudi Manongi-WHUSM
Comments
Post a Comment