PSPF YAIPATIA HOSPITALI YA TEMEKE VITANDA, MAGODORO NA MASHUKA
Afisa
Uhusiano Mwandamizi wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Bw. Abdul Njaidi,
(wakwanza kulia), akiungana na Mbunge wa viti maalum, Angela Kairuki,
(wapili kulia), mkurugenzi w manispaa ya Temeke jijini Dar es Salaam,
Photidus Kagimbo, watatu kulia), mganga mfawidhi wa hospitali ya Temeke,
Dkt. Amani Malima, (wane kulia) na Mganga Mkuu wa Manispaa ya Temeke,
Dkt. Sylvia Mamkwe, (wakwanza kushoto), wakati PSPF, ikikabidhi msaada
wa vitanda, mashuka na magodoro kwa hospitali hiyo, Desemba 7, 2015.
Msaada huo ni utekelezaji wa ahadi ya Mfuko baada ya kuombwa na Mh.
Angela Kairuki.
Na K-vis Media/Khalfan Said
MFUKO wa Pensheni wa PSPF, imeisaidia hospitali ya wilaya ya Temeke, vitanda, magodoro na mashuka ili kusaidia serikali katika juhudi zake za kupunguza uhaba wa vifaa vya hospitali za umma.
Msaada
huo ambao ni utekelezaji wa maombi ya Mbunge wa viti maalum, Angela
Kairuki, alioutoa kwa uongozi wa PSPF, baada ya kutembelea hospitali
hiyo wakati akiwa naibu waziri wa Sheria na Katiba, na kukuta akina mama
wajawazito waliofika hospitalini hapo kujifungua wengine wakilala chini
kutokana na uhaba wa viotanda, alisema Afisa Uhusiano Mwandamizi wa
Mfuko huo Abdul Njaidi na kuongeza PSPF, kwa kuwa ni Mfuko unaotoa
huduma kwa jamii nao hauna budi kutoa sehemu ya faida na kuirejesha kwa
jamii kwani wengi wao wanaofika hapo hospitali kwa ajili ya matibabu ni
wanachama wa Mfuko na wengine ni wanachama watarajiwa wa Mfuko.
Kufuatia
maombi hayo Mfuko huo umekabidhi vifaa hivyo leo Desemba 7, 2015,
ambapo Afisa Uhusiano Mwandamizi wa Mfuko huo Bw. Abdul Njaidi,
alikabidhi vifaa hivyo kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu.
Akipokea
vifaa hivyo katika hafla iliyohudhuriwa na Mkurugenzi wa Mnaispaa ya
Temeke, Photidus Kagimba, Mganga Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Dkt. Sylvia
Mamkwe, na Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Temeke, Dkt. Amani Malima,
aliishukuru PSPF, kwa moyo huo wa kusaidia jamii.
“PSPF
mmeonyesha moyo wa uungwana kwa kusaidia akina mama zetu wakati
wakisubiri kupatiwa huduma wakati wa kujifungua basi wawe na mahala
pazuri pa kulala.” Alisema
Mbunge wa viti Maalum, Angella Kairuki, (wapili kulia), akipokea msaada wa vitanda, kutoka kwa Afisa Uhusiano Mwandamizi
wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Abdul Njaidi, kwenye hosptali ya Wilaya
ya Temeke jijini Dar es Salaam Desemba 7, 2015. Mfuko huo umetoa msaada
wa vitanda, magodoro na mashuka ili kuunga mkono juhudi za serikali za
kumaliza tatizo la vifaa tiba kwenye hosipatli za umma. Kulia ni ..
Muuguzi mwandamizi wa hospitali hiyo.(P.T)
Njaidi (kulia), akiangalia wakati fundi akiunganisha moja ya vitanda hivyo wakati wa makabidhiano hayo
Njaidi akisaidiana na Muuguzi mwandamizi wa hospitali hiyo, kuweka sawa shuka kwenye kitanda
Mh.
Angela Kairuki, (wapili kulia), akimsikiliza Afisa Uhusiano Mwandamizi
wa PSPF, Bw. Abdul Njaidi, wakati wakibadilishana mawazo kabla ya
kukabidhi vifaa hivyo. Wengine kushoto ni maafsia wa PSPF
Mh. Kairuki akipatiwa maelezo juu ya huduma zilizochapishwa kwenye kipeperushi cha PSPF
Mh. Angela Kairuki akitoa hotuba yake wakati wa kupokea na kukabidhi msaada huo
Mh. Angela Kairuki akitoa hotuba yake wakati wa kupokea na kukabidhi msaada huo
Mganga mkuu wa wilaya ya Temeke, Dkt. Sylvia Mamkwe, akitoa nasaha zake
Mh.
Kairuki (kulia), akijadiliana jambo na mafisa wa hospitali ya Temeke na
uongozi wa wilaya pamoja na Afisa Uhusiano wa PSPF, Bw. Njaidi
Wafanyakazi wa hospitali hyo wakibeba sehemu ya vitanda hivyo
Mkuu wa wilaya ya Temeke, Bi. Sophia Mjema, akipena mikono na Bw. Njaidi wakati akimshukuru kwa msaada huo
chanzo:mjengwa
Comments
Post a Comment