COSOTA, CMEA kuanza kulipa wanamuziki mirahaba Januari 2016



Afisa Mtendaji Mkuu wa Chama Cha Hakimiliki Tanzania (COSOTA) Doreen Sinare akielezea umuhimu wa wanamuziki kujisajili kwao kupitia Kampuni iliyopewa jukumu la kuendesha zoezi usajili, Copyrights Management East Africa Limited (CMEA) ilikuweza kupata haki zao kutokana na kazi zao.
Chama cha Hakimiliki Tanzania (COSOTA) kwa kushirikiana na kampuni ya kusimamia kazi za wanamuziki nchini Copyrights Management East Africa Limited (CMEA) wataanza kulipa mirabaha ya wanamuziki na wadau wake kuanzia mwakani.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Cosota, Doreen Sinare alisema kuwa wanamuziki, watunzi na ma’producer’ watalipwa asilimia 60 kwa kila wimbo au video itakayochezwa katika redio na televisheni yoyote ndani na nje ya nchi kwa kutumia vifaa bora vilivyowekwa na kampuni ya CMEA.

Doreen alisema kuwa manamuziki, msanii alitakiwa kupata asilimia 70 ya kazi yake, lakini asimilia 10 itakatwa katika malipo hayo na kuingia katika mifuko ya jamii kwa mahitaji yake ya baadaye.

Alisema kuwa wanamuziki ni sawa na wafanyakazi wengine na asilimia 10 hiyo itamwezesha kujipatia kipato chake kama ilivyo kwa wafanyakazi wengine katika taasisi mbalimbali.

Kwa mujibu wa Sinare alisema kuwa ili kuhakikisha kila mwanamuziki anafaidika na kazi yake, watashirikiana na vyama vingine vya Hakimiliki katika nchi mbali mbali kwa kutumia hati ya malipo zinazotokana na bei za matangazo kwa televisheni na vituo vya redio.

Alisema kuwa Cosota na CMEA pia watawapa ushirikiano vyama hivyo ili nao waweze kupata haki za malipo ya wanamuziki wao kwa vituo vya televisheni na redio vitakavyotumia kazi za wanamuziki wa nje.

“Lengo la Cosota na CMEA ni kuona wasanii wanafaidika na kazi zao, mirabaha ya kwanza tutaanza kulipa Januari 2 na kwa sasa tupo katika hatua za mwisho kukamilisha jinsi tutavyolipa, ndiyo maana tumetoa semina kwa wanamuziki, lengo ni kuwahamasisha kujisajili,” alisema Sinare.

Afisa Mtendaji Mkuu wa CMEA, Paul Matthysse alisema kuwa mbali ya wanamuziki, kampuni yao itawawezeha pia watayarishaji wa muziki na wasanii wengine pamoja na vyombo vya habari kupata kufahami takwimu sahihi za nymbo zilizochezwa kwa siku, wiki, mwezi na kwa mwaka.

Matthysse alisema kuwa kampuni yao imewekeza mitambo ya kisasa inayowezesha kuchapisha na kuhakiki nyimbo pindi zinapochezwa hewani na televisheni na redio na kutoa ripoti za aina mbalimbali zinazohitajika kutumika kwa malengo maalum.

“Pia tunapokea na kuhifadhi nyimbo kwenye mitambo maalum kwa matumizi ya uhakiki, na kudhibiti kiasi cha mirabaha ambacho Cosota kupitia vyombo vya habari inatakiwa kuwalipa wasanii kulingana na idadi kamili ya urushwaji wa kazi zao,” alisema Matthysse.

Alisema kuwa wanamuziki na wasanii wengine ambao hawatakuwa na usajili, watakosa haki zao pamoja na CMEA kuendelea kurekodi kazi zao zinazochezwa katika redio na televisheni mbali mbali. “Ni muhimu kwao kujisajili, kutojisajili ni kupoteza haki zao zinazotokana na kazi yako,” alisisitiza.
Mkuu wa Uendeshaji wa kampuni ya CMEA, Abdi Zagar akielezea jinsi ya mfumo wa kisasa wa ukusanyaji taarifa za wanamuziki kwenye vituo vya televisheni na redio kwa ajili ya kutumiwa na Cosota ili kufanya malipo sahihi kwa wanamuziki na wadau wake.
Mwanamuziki, Barnaba akitoa maada katika semina hiyo iliyoandaliwa na Cosota na CMEA kwa ajili ya kuwapa elimu wanamuziki na wadau wake kuhusiana na malipo ya mirahaba.
Mkurugenzi wa vipindi wa Clouds Media Group, Ruge Mutahaba akijibu moja ya maswali katika semina hiyo. Mutahaba aliwahamasisha wanamuziki kujisajili CMEA kwa lengo la kupata haki kutokana na kazi zao.
Wanamuziki wa muziki wa dansi, Chalz Baba na Jonico Flower wakifuatilia semina hiyo ambayo iliwapa somo kuhusiana na umuhimu wa kujisajili kupitia kampuni ya CMEA na Cosota ili kufaidika na kazi zao.
Afisa Mtendaji Mkuu wa CMEA, Paul Matthysse akifafanua jambo kuhusiana na faida za wanamuziki na wadau wake mara baada ya kujisajili na kuanza kulipwa fedha zao

Comments

Popular posts from this blog

PATA UKWELI KUHUSU MWANAMALUNDI, MTU WA MAAJABU ALIYEWAHI KUTOKEA KATIKA HISTORIA YA KABILA LA KISUKUMA