WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI YAFUTA VYAMA VYA KIJAMII 1,268
Msemaji
wa Wizara Mambo ya Ndani ya Nchi, Isaac Nantanga akizungumza na
waandishi wa habari leo juu ya ufutaji wa vyama vya kijamii
vilivyoshindwa kuendesha pamoja na kushindwa kulipa ada, kushoto ni
Mwanasheria wa wizara hiyo, Berious Nyasembwa.
Waandishi wa habari wakifatilia taarifa ya Msemaji wa Wizara Mambo ya Ndani ya Nchi, Isaac Nantanga leo jijini Dar es Salaam.
Picha na Avila Kakingo wa Globu ya Jamii.
Na Zainabu Hamisi, Globu ya Jamii.
WIZARA ya
Mambo ya Ndani ya Nchi imefuta vyama vya Kijamii 1,268 kutokana na
kushindwa kutekeleza majukumu yao na sheria zilizowekwa katika
uendeshaji wa vyama pamoja na mashirika yasiyo ya Kiserikali (NG’0s).
Akizungumza
na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Msemaji wa Wizara ya
Mambo ya Ndani, Isaac Nantanga amesema kuwa kufutwa kwa vyama hivyo ni
kutokana na kukiuka masharti ya uwendeshaji wa taasisi ikiwemo kutolipa
ada kwa mujibu wa sheria.
Katika
ufutwaji wa vyama hivyo chama kimojawapo kilichofutwa ni chama cha
wapiga picha nchini ambacho kimeshindwa kukidhi vigezo vya uendeshaji na
kushindwa hata kuendesha vikao vyake.
Nantanga
amesema kuwa vyama vingine 1,406 vimepewa kusudio la kufutwa na baada
siku 21 kuanzia leo, kama havitatoa kusudio la kujitetea basi navyo
vitafutwa.
Amesema
kufuatana na kanuni ya vyama inayoundwa na kifungu cha 38 cha sheria ya
vyama vyote vya kijamii vinapaswa kulipa ada ya kila mwaka.
Aidha,
amesema kanuni ya 6 za vyama za kijamii inayosomwa pamoja na kifungu cha
22 cha sheria ya vyama inavitaka vyama vya kijamii kuwasilisha taarifa
za kila mwaka za hesabu zilizokaguliwa za mapato na matumizi ya vyama
kwa msajili wa vyama.
Aliongeza
kuwa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi inatoa angalizo kwa vyama vyote
vya kijamii kuendesha shughuli zake kwa kufuatana na sheria
zilizoanzisha vyama hivyo.
Comments
Post a Comment