Shule zote Los Angeles zafungwa ghafla
Shule zote Los Angels zafungwa ghafla
Shule zote za uma katika jimbo Los Angeles Marekani zimefungwa mara moja kufuatia tishio la usalama.
Tangazo hilo lilitolewa na muungano wa wakuu wa shule zote za umma unaathiri takriban shule 1,000.
Takriban
wanafunzi laki 700,000 walilazimika kurejea makwao baada ya tishio
ambalo kufikia sasa halijatangazwa wazi kupokewa na maafisa wa Polisi.
Yamkini
ujumbe wa kuwatahadharisha umma ulipatikana kwa njia ya kielektroniki na
hivyo ikawalazimu kuamuru wanafunzi wote waondoke ilikufanikisha
shughuli ya kutafuta na kusaka tishio lililoko.
Tahadhari hiyo ya umma imetokea wiki mbili tu baada ya mauaji ya watu 14 katika kituo cha San Bernardino.
Watu hao walipigwa risasi na mume na mkewe ambao wanashukiwa kuwa walishawishiwa na waislamu wenye itikadi kali ughaibuni.
Takriban wanafunzi laki 700,000 walilazimika kurejea makwao
Polisi
tayari wameanza kupekua maeneo yanayoshukiwa kuwa na hatari na wanasema
kuwa shule zote zitasalia zimefungwa hadi tishio hilo litakalo ondolewa.
Afisa
anayesimamia usalama wa shule za umma Steven Zipperman, amesema kuwa
idara hiyo ilipokea tishio kwa njia ya kielektroniki mapema hii leo ndio
sababu wakaamuru shule zikafungwa.
''tumeamua kufunga shule hadi pale tutakapobaini kuwa ni salama''
Mmoja wa
maafisa wakuu usalama ambaye hakutaka jina lake litajwe anasema kuwa
tishio hilo lilipokewa kupitia barua meme iliyotumwa kwa mmoja wa
maafisa wanaosimamia shule Los Angeles kutoka ughaibuni.BBC
Comments
Post a Comment