Jinsi ya kuripoti ikiwa umetozwa nauli isiyo sahihi
Je, UMETOZWA NAULI KUBWA KWENYE BASI KULIKO UMBALI UNAOKWENDA?
Fanya yafuatayo:
- Bishia nauli uliyotozwa kuwa si halali. mfano kama unakokwenda ni Dar-Mafinga, nauli inapaswa kuwa 20,000 wewe ukatozwa Dar - Njombe 25,000, bishia. Kondakta akikataa lipa, ingia kwenye gari.
- Atakupa tiketi imeandikwa Dar - Mafinga 25,000 au atakupa tiketi imeandikwa Dar-Njombe 30,000. Pokea
- Ipige picha hiyo tiketi, au iscan kisha itume kwenda nambari 0682 887722(kwa whatsapp, telegram au wechat) ukielezea kuwa umetozwa nauli kubwa kuliko umbali wa safari au umepandishwa bus ordinary wakati wewe ulitozwa nauli ya luxury. Na kwamba kondakta amekataa kukuandikia tiketi ya unakokwenda badala yake akakuandikia tiketi inayoonesha kituo ambacho basi linaishia. Au Tuma ujumbe au piga simu kwenda 0800 110 019 au 0800 110 020 (bure). Namba hizi tumia hata pale gari inapokatisha ruti au kuwatelekeza njiani baada ya kuharibika.
- Basi litasimamishwa kituo cha mbele, utarudishiwa nauli yako. Kama limekamatwa na askari polisi basi dereva au kondakta atarudisha nauli na 30,000 itamhusu. Akikamatwa na SUMATRA basi atarudisha nauli na faini ya sh.250,000 itamhusu.
Imetolewa na
RSA TANZANIA
USALAMA BARABARANI JUKUMU LETU SOTE
Comments
Post a Comment