Tanesco yawafukuza kazi wafanyakazi 7 kwa ubadhilifu
Uongozi
wa shirika la umeme nchini Tanesco umewafukuza kazi wafanyakazi saba
waandamizi wa shirika hilo wakiwemo mameneja kutokana na makosa
mbalimbali ikiwemo vitendo vya wizi, kudai rushwa, ubadhirifu wa mali wa
shirika hilo pamoja na kutoa lugha chafu kwa wananchi jambo ambalo ni
kinyume na taratibu za maadili ya kazi na uongozi huo kuwaonya
wafanyakazi wengine wenye tabia kama hizo kwamba watachukuliwa hatua.
Mkurugenzi
mkuu wa shirika hilo Mhandisi Felichesm Mramba akitoa taarifa juu ya
uumuzi wa kufukuzwa kazi kwa wafanyakazi hao saba kwa waandishi wa
habari jijini Dar es Salaam amesema uamuzi huo umechukuliwa ikiwa ni
mpango endelevu wa shirika la Tanesco kuimrisha nidhamu kwa wafanyakazi
wake kutambua wajibu wao wa kutoa huduma ya nishati kwa wananchi na sio
na sio kuwasumbua wateja na kutaja vitengo ambavyo wafanyakazi hao
wamefukuzwa ikiwemo ngazi ya mameneja, wahandisi na wahasibu kutoka
mikoa ya Kinondini kaskazini, Katavi, Kagera na Ilala.
Akiendelea
kutoa taarifa juu ya utekezaji wa kusanyaji wa mapato ili kuendesha
shirika hilo kwa ufanisi unaotakiwa kwa sasa mhandisi Mramba ametoa siku
saba kwa wateja ambao wanalihujumu shirika la umeme kwa kujiunganishia
umeme kwa wizi kujisalimisha wao wenyewe kutokana na kuanza kwa
operesheni maalumu ya nyumba kwa nyumba kuhakiki mita ili kubaini
upotevi wa nishati ya umeme inayotumika bila kulipiwa mpango ambau
utahusisha jeshi la polisi katika kuwakamata wahalifu wote na mali zao
sasa kunadiwa wakishindwa kulipa faini.
Pamoja na
mambo mengine mkurugenzi mkuu huyo wa Tanesco amesema mpango wa
uzalishaji wa nishati ya umeme kwa kutumia vyanzo vya gesi tokea mwezi
septemba mwaka huu umesaidia kuongeza megawati 300 kutoka megawati 260
hivyo hatua hiyo kuchangia kuboresha hali ya umeme hapa nchini na kuwa
na matarajio ya kupata megawati 700 ifikapo mwezi januari mwakani
kupitia umeme wa nishati ya gesi.(P.T)
Comments
Post a Comment